Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa hawza nchini Iran, katika mkutano wake na Dkt. Barzouei, Rais wa Chuo Kikuu cha Walimu, uliofanyika katika ofisi yake, aliwashukuru wahusika wa chuo hicho kwa juhudi na huduma zao, akakieleza chuo hicho kuwa moja ya taasisi muhimu zaidi za kimkakati nchini katika nyanja ya utamaduni, elimu na malezi, na akasisitiza umuhimu wa mageuzi ya kina katika vipengele na programu za malezi ya walimu.
Mkuu wa taasisi za elimu ya dini, huku akirejelea msisitizo maalumu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu suala la malezi ya walimu, alisema: huduma za Chuo Kikuu cha Walimu zinathaminiwa na kazi ya chuo hiki ni miongoni mwa masuala yanayosisitizwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Akirejelea hatua zilizochukuliwa katika miundombinu na maendeleo ya majengo ya chuo hicho, alisema: kuhakikisha faraja, utulivu na hadhi ya wanafunzi-walimu ni jambo lisilopingika, na kupuuzia mazingira ya maisha na elimu ya wale wanaotarajiwa kuwa viongozi wa elimu na malezi ya nchi hakukubaliki.
Mkuu wa taasisi za elimu ya dini, huku akisisitiza umuhimu wa usanifu wa Kiislamu katika vituo vya elimu, alisema: usanifu wa jadi wa Kiislamu unatokana na maana, dhikr na maarifa ya kina ya kidini, na unaweza kwa wakati mmoja kuleta uchangamfu, utulivu na malezi ya kiroho. Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu, licha ya maendeleo mengi, bado hatujaweza kuunda mifumo mipya ya usanifu wa Kiislamu inayolingana na mahitaji ya leo.
Mjumbe wa wanazuoni wa Baraza la Walinzi wa Katiba aliongeza kuwa; katika miradi ya ujenzi ya Chuo Kikuu cha Walimu, ziundwe kamati za pamoja za tafakuri zikijumuisha wataalamu wa hawza na wa vyuo vikuu ili kuanzia hatua ya usanifu hadi utekelezaji, kuzalisha mifumo ya kina, ya kielimu na yenye kuhamasisha.
Ayatullah A‘rafi, akirejelea mabadiliko makubwa ya kijamii na kiutamaduni ya miongo ya hivi karibuni, alisisitiza kuwa: mifumo na mbinu za sasa za malezi na utamaduni, ingawa zimekuwa na manufaa, hazijitoshelezi kukabiliana na changamoto na hali za kizazi kipya. Leo tunakabiliwa na kizazi ambacho kwa kiasi fulani kimekumbwa na mpasuko katika misingi ya pamoja, na uwezo wa ushawishi wa mbinu za jadi umepungua.
Aliongeza kwa kusena: Chuo Kikuu cha Walimu kinapaswa kuwa mstari wa mbele katika kubuni mifumo mipya ya malezi — mifumo iliyo ya kina, yenye athari, isiyo ya moja kwa moja, na inayojengwa juu ya mapenzi na uelewa sahihi wa ulimwengu wa maisha ya kizazi cha vijana.
Mkuu wa taasisi za elimu ya dini, huku akisisitiza nafasi ya msingi ya mwalimu katika kutatua matatizo ya kiutamaduni ya nchi, alisema: ikiwa mwalimu mwema, mjuzi na mwenye uwezo atalelewa, hata katika mazingira rahisi kabisa anaweza kuleta mabadiliko; lakini hata kama vifaa bora vitatolewa bila kumlea mwalimu anayestahili, matokeo yanayotakiwa hayatapatikana.
Akirejelea umuhimu wa “kuujua Ulimwengu wa Magharibi kwa mtazamo wa haki na wa kukosoa” katika mfumo wa malezi ya walimu, alisema: mwalimu lazima awe na uelewa kuhusu misingi ya kifalsafa, kiutamaduni na kifikra ya ustaarabu wa Magharibi; asiingie katika kuvutiwa kupita kiasi wala katika kuukanusha bila haki. Hili ni moja ya mapungufu katika mfumo wa sifa za kitaaluma za walimu.
Ayatullah A‘rafi pia alisisitiza umuhimu wa wanafunzi-walimu kukutana na shakhsia kubwa za kielimu, kiroho na kimapinduzi, na akasema: hata kukutana mara moja au mbili kwa kina na watu wakubwa kunaweza kuwa na athari ya kudumu ya kimalezi; jambo ambalo leo ni gumu kulitekeleza lakini ni muhimu.
Mjumbe wa wanazuoni wa Baraza la Walinzi wa Katiba aliongeza: kuzingatia historia ya utamaduni, ustaarabu wa Kiislamu, historia ya sayansi na historia ya kisasa ya Mapinduzi ya Kiislamu kunapaswa kufuatiliwa kama sehemu muhimu ya programu ya malezi ya walimu.
Msaada wa taasisi za hawza kwa Chuo Kikuu cha Walimu
Mkurugenzi wa hawza, akitangaza utayari kamili wa hawza kushirikiana na Chuo Kikuu cha Walimu, alisema: Wizara ya Elimu na Malezi pamoja na Chuo Kikuu cha Walimu ni miongoni mwa vipaumbele vyetu vikuu, na katika kila kiwango tutakachoweza, tutakuwa pamoja nao kwa msaada wa kifikra, ushauri, kisayansi na kisheria.
Mwisho, Ayatullah A‘rafi alisisitiza kuwa: ikiwa mwalimu atalelewa ipasavyo, sehemu kubwa ya matatizo ya kiutamaduni, kijamii na hata kiuchumi ya nchi yatatatuliwa, na huu ndio uwekezaji muhimu zaidi wa kimkakati kwa mustakabali wa Iran.
Maoni yako