Jumapili 4 Januari 2026 - 00:00
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Pakistan ashiriki katika Kongamano la Dunia la Dini, Bangkok – Thailand

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hassan Meethami alishiriki katika Kongamano la Kimataifa la Dini huko Bangkok, Thailand, ambapo alikutana na viongozi wa dini mbalimbali na akasisitiza jukumu la uwajibikaji la viongozi wa kidini, kuimarisha kuishi kwa amani, na kupanua ushirikiano wa kitamaduni na kitaasisi kati ya nchi mbalimbali.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hassan Meethami, Rais wa Akademia ya Zahra (s.a.) ya Pakistan na Katibu Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, kwa mwaliko rasmi wa waandaaji, alihudhuria Kongamano la Dunia la Kidini  lenye kichwa cha habari kisemacho: “Nafasi na Majukumu ya Viongozi wa Kidini kwa kuzingatia Changamoto za Kisasa za Kimataifa”, lililofanyika katika mji wa Bangkok, Thailand, na akatoa hotuba.

Kwa mujibu wa taarifa hii, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shabbir Hassan Meethami, pembezoni mwa kongamano hili, alifanya mikutano na mazungumzo mbalimbali na wanazuoni, wanafikra na viongozi wa dini tofauti, na akasisitiza umuhimu wa kuimarisha kuishi kwa amani, mazungumzo yenye kujenga, na ushirikiano wa dini katika kukabiliana na migogoro ya kimataifa.

Katika mwendelezo wa safari hii, akiwa ndani ya muktadha wa shughuli za “Taasisi ya Njia za Kisheria za Sadiq”, alikutana na Dkt. Mohammad Mahdi Imanpour, Rais wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu, pamoja na Mheshimiwa Nasiruddin Haidari, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Thailand, na wakabadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu ya kitamaduni, kidini na ushirikiano wa pamoja.

Katika mikutano hiyo, kwa kutoa shukrani kutokana na jukumu chanya la Baraza Kuu la Kiislamu la Thailand na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukuza mazungumzo ya kidini na mwingiliano wa kitamaduni, alisisitiza umuhimu wa kuendeleza uhusiano wa vitendo na wa kitaasisi kati ya Pakistan na Iran, akisema: Kuimarisha ushirikiano uliopangwa na wenye muundo kati ya nchi hizi mbili ni hitaji la msingi la wakati wa sasa, na kunaweza kuleta faida pana kwa mataifa ya nchi zote mbili.

Aidha, kwa kusisitiza ulazima wa kuimarisha mshikamano wa kimadhehebu na wa kidini kati ya dini mbalimbali, aliitaja nafasi ya viongozi wa kidini katika kueneza amani, uadilifu na kuishi kwa amani kuwa ni ya msingi na yenye kuamua kwa kiasi kikubwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha