Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kwa mtazamo wa wataalamu wengi wa masuala ya kimataifa, kuchapishwa kwa hati ya mkakati wa usalama wa taifa wa Marekani — ambayo ni miongoni mwa nyaraka kuu katika nyanja ya usalama wa taifa na sera ya kigeni ya Marekani na huchapishwa kila baada ya miaka minne — ni ushahidi ulio wazi kuliko chochote kingine unao onesha kudorora kwa Marekani kwenye sekta ya ushawishi wake katika mpangilio mpya wa dunia.
Ukweli mchungu kwa Marekani kwa mujibu wa maudhui ya hati moja
Masoud Barati, mwandishi wa habari, anaamini katika muktadha huu kwamba: mwanzoni mwa hati, serikali ya Trump inazitaja sera za zamani za Marekani kuhusu masuala ya kimataifa kuwa zilikuwa potofu na zinazopita uwezo wa Marekani.
“Walizidisha tathmini ya uwezo wa Marekani wa kufadhili kwa wakati mmoja serikali kubwa ya ustawi–udhibiti–utawala pamoja na mkusanyiko mkubwa wa kijeshi, kidiplomasia, kiintelijensia na misaada ya nje.”
Hati hiyo pia inashambulia sera ya “biashara huria” na kuitaja kuwa sababu ya kutoweka kwa “tabaka la kati” na “ubora wa kiuchumi na kijeshi” wa Marekani. Kwa upande mwengine, hati hii inakiri kwamba Marekani katika ulimwengu wa sasa haina ubora wa kiuchumi wala wa kijeshi.
Aidha, alisisitiza kuwa mambo ambayo hati ya mkakati wa usalama wa taifa wa Trump inayaita makosa, yalikuwa vipengele vikuu vya kuunda utawala wa Marekani na mpangilio wa Kimarekani baada ya Vita ya Pili ya Dunia, hususan baada ya kusambaratika kwa Umoja wa Kisovieti. Hati ya Trump kwa uwazi na mara kwa mara inairejesha Marekani ndani ya mipaka yake, na ni wazi kwamba Trump haioni hali ya Marekani kuwa imara na yenye nguvu kiasi cha kuweza kuendeleza sera za zamani. Hata anapozungumzia sera za Marekani kuhusu Asia ya Magharibi (Mashariki ya Kati), anaonesha kufurahishwa na ukweli kwamba masuala ya eneo hili hayatawaliwi tena sera ya kigeni ya Marekani, na kwamba vita visivyo na mwisho vya “kujenga mataifa” vimefikia tamati.
Mbinu ya kuhifadhi mizani ya madaraka imebadilika kabisa
Aliendelea kusema: katika sehemu nyingine ya hati hii, “kuimarisha nguvu ya viwanda” kumetajwa kuwa kipaumbele cha juu kabisa cha sera ya uchumi wa taifa, na cha kuvutia ni kwamba serikali ya Trump inaona hili kuwa sharti la kurejesha nguvu ya kitaifa ya Marekani iliyopotea. Kauli hii yenyewe inaonesha kuwa Trump haoni uwezo wa sasa wa viwanda wa Marekani kuwa wa kutosheleza mahitaji ya nchi hiyo wakati wa amani na vita.
Barati pia alisema: kipengele kingine muhimu cha hati hii ni namna inavyokabiliana na suala la kuongezeka kwa nguvu kwa wahusika wengine katika uwanja wa kimataifa. Zamani iliaminika kuwa Marekani inalenga kuwazuia wahusika wapya kwa kiwango cha juu kabisa. Jambo hili lilikuwa likielezwa kwa istilahi kama mhimili wa mamlaka ya kiimla, mhimili wa mabadiliko au “kreen”, lakini katika hati hii msisitizo uko kwenye kulinda “mizani ya madaraka”. Wakati huohuo, hati inasisitiza kwamba Marekani haiwezi kuruhusu taifa lolote kupata ushawishi mkubwa kiasi cha kuhatarisha maslahi ya Marekani, lakini njia iliyopendekezwa ni kushirikiana na washirika ili kuhifadhi mizani ya madaraka. Huu si mkabala wa kiwango cha juu kabisa, bali ni kuukubali ukweli wa kuongezeka kwa nguvu kwao na kujikita tu katika kuzuia kutawaliwa kwao. Kwa maneno mengine, ni lazima kukiri kwamba Marekani imekubali mabadiliko ya mfumo na mlingano wa madaraka katika uwanja wa kimataifa.
Mabadiliko ya mpangilio wa dunia na kuendelea kudorora
Kwa mtazamo wa Dkt. Fouad Izadi, mtaalamu na mchambuzi wa sera za kimataifa, Marekani si kwamba imeanza kudorora leo au jana, bali kwa miaka mingi imekuwa katika mkondo wa kudorora; jambo ambalo hata katika ripoti za kila mwaka za baadhi ya mikutano na makongamano muhimu kama Mkutano wa Munich, limeelezwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Akirejea kauli za Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, ambaye mara kadhaa katika hotuba mbalimbali ameeleza mchakato wa kudorora kwa Marekani kuwa ni wa kweli na usioweza kurekebishwa, alisema: ukweli ni kwamba Mapinduzi ya Kiislamu tangia mwanzo yalipinga utawala wa Mashariki na Magharibi, na leo pia yana uhasama na Marekani si kwa sababu ya asili ya nchi hiyo, bali kwa sababu ya sera zake za kibeberu na za kidhalimu ambazo kwa takriban miongo mitano iliyopita zimekuwa zikiendelea dhidi ya nchi yetu.
Tuwe waangalifu na malengo ya vita vya kiutambuzi vya adui
Izadi, akibainisha kwamba vita vya kiutambuzi vya adui — hasa kutoka kwa wanasiasa wa Marekani — vinaendeshwa kwa lengo la kupandikiza dhana ya kushindwa Jamhuri ya Kiislamu na matokeo yake kupandikiza kukata tamaa kuhusu mustakabali miongoni mwa watu na kizazi cha vijana, alisisitiza: lililo muhimu ni kuwa waangalifu tusimtangaze kwa makusudi adui na vyombo vyake vya habari, na tathmini zetu kuhusu Marekani ziwe za kweli na zenye kuzingatia tajriba za nyuma; huku tukitambua kwamba kudorora kwa Marekani, kwa mujibu wa kauli za wachambuzi wao wenyewe, ni jambo la hakika.
Dalili kubwa za kusambaratika kutoka ndani
Dkt. Mohammad Sadeq Khorsand, mhadhiri na mtafiti wa masuala ya kisiasa, naye akirejea kwamba kile kinachoendelea sasa katika nyanja mbalimbali nchini Marekani si kudorora tu, bali ni dalili za kusambaratika, alisema: kwa mujibu wa tahadhari za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa Kimarekani, nchi hiyo inakabiliwa na matatizo na changamoto nyingi za kijamii. Hata think tank ya Atlantic Council muda mfupi uliopita ilitangaza wazi kwamba kwa upande wa masuala ya kijamii, Marekani iko katika kiwango cha chini kabisa.
Akiendelea kufafanua kwamba katika hali ya sasa, mfumo wa kimataifa hauna uongozi mmoja na mahususi, bali una nguvu mbalimbali, alisema: mifumo ya kimataifa imepitia hoja na hali tofauti hadi sasa, na cha kuzingatiwa ni kwamba; nguvu na ustaarabu mbalimbali, baada ya kipindi cha kuonesha mamlaka, vipo katika hatua huporomoka na kudidimia.
Kuongezeka kwa migawanyiko ndani ya jamii ya Marekani
Mchambuzi huyu wa masuala ya kisiasa na kimataifa aliongeza kusema: Bila shaka katika muktadha huu kuna vigezo vinavyoonesha kuwa mfumo wa dunia ya leo si wa nchi moja tena; hivyo, masuala ya kiuchumi, kitamaduni, kisiasa na mengineyo yanapaswa kuchunguzwa na kuchambuliwa. Think tank ya Atlantic Council muda mfupi uliopita ilitoa ripoti yenye kichwa cha habari kisemacho: “Dola inayoshindwa”, ambayo ilieleza kuwa; kwa upande wa kijamii na kiwango cha kukubalika, Marekani iko katika hali ya chini kabisa, na kwamba migawanyiko ya kisiasa, kijamii na kitamaduni iliyopo ndani ya nchi hiyo itaongezeka na kuwa mikubwa zaidi katika siku za usoni.
Maoni yako