Jumapili 7 Desemba 2025 - 11:00
Wafanyakazi Katika Kampuni ya Ndege ya AirAsia Watavaa Hijabu

Hawza/ kampuni ya ndege ya AirAsia ambayo inajumuisha nchi kadhaa za Asia ikiwemo Indonesia, imetangaza kwamba kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2026 wafanyakazi wake wa kike watavaa sare inayojumuisha hijabu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kampuni ya ndege ya AirAsia katika taarifa yake imesema kuwa; uamuzi huu umechukuliwa kwa kuzingatia maoni na mrejesho uliokusanywa kutoka kwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, kwa kuwa lengo la kampuni hii ni kuweka mazingira ya kazi ambayo kila mfanyakazi anaweza kufanya kazi kwa kujiamini, kwa faraja na kwa moyo uliojaa fahari.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo alisema: “Ninaona uamuzi huu kama hatua ya maendeleo ambayo itatuwezesha kusaini mikataba na nchi zaidi ambazo kuvaa hijabu ni sehemu ya imani zao.”
Uamuzi huu utaanza kutekelezwa mwaka 2026 na sare sahihi yenye hijabu kwa ajili ya wafanyakazi wa ndege wanawake ipo katika hatua ya kubuniwa na kushonwa.
Chanzo: kinihalal.com

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha