Jumapili 7 Desemba 2025 - 10:00
Wananchi wa Ujerumani, Wapinga Safari Aliyoifanya Waziri Mkuu wa Nchi Hiyo ya Kusafiri Kwenda Israel

Hawza/ Wanaharakati wanao ihami Palestina na wanachama wa kundi la Amnesty International, siku ya Ijumaa waliandaa maandamano katika kituo cha Berlin, yakiwa na lengo la kupinga safari iliyopangwa awali ya Friedrich Merz, Waziri Mkuu wa Ujerumani, kwenda Israel katikati ya uhalifu wa kivita unaoendelea Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wanaharakati wa haki za binadamu walikusanyika katikati ya Berlin na kuweka mfano wa tanki mbele ya lango la Brandenburg, ili kudai kusitishwa kwa usafirishaji wa silaha za Ujerumani kwenda Israel. Walibeba mabango yaliyoandikwa “Silaha si zawadi kwa wahalifu wa kivita” na “Kutuma silaha kwa ajili ya uhalifu wa kivita na mauaji Ghaza ni marufuku.”
Kundi hili pia lilionesha upinzani wao kutokana na mkutano alioufanya Waziri Mkuu wa Ujerumani pamoja na maafisa wa Israel na kuuita kuwa ni “fedheha.”
Müller Falbush alisema: “Leo tuko hapa kulipinga hili kwa uwazi, na kwa sauti kubwa kusema kwamba; hakuna uhusiano wowote na Israel ulio wa kawaida.”
Akaendelea kusema: Waziri Mkuu anajifanya kana kwamba kila kitu Ghaza ni cha kawaida, ilhali uhalifu na mauaji yanayofanywa na utawala wa Kizayuni bado yanaendelea huko Ghaza.
Chanzo: Shirika la Habari Anadolu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha