Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wizara hiyo pia imewataka wanachama wote wa magenge ya kihalifu na wale wanao shirikiana na Israel wajisalimishe mara moja.
Wizara hiyo imepongeza misimamo ya koo za Kipalestina ambazo zimetangaza kuondoa msaada wao kwa makundi hayo, na ikaongeza kuwa msimamo huo unazidisha juhudi za kulinda safu ya ndani katika Ukanda wa Ghaza.
Wizara hiyo pia imethibitisha kifo cha Yaser Abushabab mhalifu, na kukitaja kuwa ni mwisho usioweza kuepukika kwa yeyote anayetaka kuwa chombo cha uvamizi wa Israel dhidi ya watu wake. Wizara hiyo imeeleza kwamba; ahadi ya Israel dhalimu kuhusiana na kuyalinda makundi haya ya wasaliti haitadumu kwa muda mrefu, na hivi karibuni wataangukia katika mtego wa mauti.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa; Israel haijafanikiwa kudhoofisha umoja na mshikamano wa kijamii wa watu wa Palestina, wala kuleta mpasuko katika muundo wa kijamii wa watu hawa. Magenge ya kigaidi yaliyoanzishwa na wavamizi kwa lengo la kuharibu usalama wa ndani yamekuwa yakitengwa, hayana msaada wowote kwa wananchi au kijamii, na hivi karibuni yatatoweka.
Chanzo: Tovuti ya Habari Kuu ya Palestina
Maoni yako