Jumapili 7 Desemba 2025 - 07:00
Ardhi ya Mitume Imetapakaa Damu ya Waliodhulumiwa, na Dunia Imenyamaza

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika ujumbe wake, alisisitiza kuwa licha ya kuwepo kwa kile kinachoitwa makubaliano ya amani ya kulazimishwa, uvamizi na uhalifu wa Uzayuni bado unaendelea. Alibainisha kuwa kwa ajili ya kuilinda, kuongea pekee hakutoshi; bali kuna haja ya kuchukua hatua za kivitendo na zenye uzito.

Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia nchini Pakistan, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa Siku ya Dunia ya Udongo, akirejea muendelezo wa dhulma ya utawala wa Kizayuni, alisema kuwa; licha ya jina la amani ya kulazimishwa, mashambulizi na uhalifu wa utawala huo bado unaendelea, na kwamba kwa kulihifadhi sayari yetu, haitoshi kutoa tamko bila kuchukua hatua stahiki.

Katika ujumbe huo imeelezwa: Ardhi ya mitume imelowa damu ya wanyonge, na licha ya kile kinachotangazwa kuwa ni makubaliano ya amani ya kulazimishwa, utawala wa Kizayuni, kwa msaada wa madola ya kikoloni, unaendelea kutekeleza uhalifu wa kinyama na mauaji ya kikatili.

Akirejea kupitishwa kwa azimio jingine katika Umoja wa Mataifa kuhusu kusitishwa kwa mapigano Ghaza, ameongeza kuwa; taasisi za kidini na kijamii za Palestina, wanaharakati wa kujitolea, pamoja na waandishi wa habari, wamelengwa na kuuawa kwa njia ya kuchagua, huku Umoja wa Mataifa ukiridhika tu na kutoa azimio za kulaani. Alisisitiza kuwa sasa ni wakati wa kupita hatua ya matamko, na kuchukua hatua madhubuti za kivitendo kwa ajili ya kuilinda Dunia.

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Pakistan, akisisitiza umuhimu wa Siku ya Dunia ya Udongo, alibainisha kuwa maadhimisho haya ni fursa ya kukumbusha wajibu wa kuilinda ardhi dhidi ya uchafuzi na uharibifu, na kuzuia matumizi mabaya na ya unyonyaji ya rasilimali za udongo. Miongoni mwa hatua muhimu alizotaja ni: kuboresha mifumo ya mifereji ya maji, kurekebisha ardhi iliyokumbwa na mmomonyoko, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuchukua hatua za haraka za kuhifadhi mazingira.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha