Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Ridha Kakavand, Afisa Masuala ya Utamaduni na Mitandao wa Kampuni ya Tavanir, katika ziara yake ya kutembelea Shirika la Habari la Hawza na katika kikao na mhariri mkuu pamoja na wahariri wa chombo hiki cha habari, aliitaja sekta ya habari kuwa chombo chenye nguvu zaidi katika “jihadi ya kubainisha ukweli”, na akirejelea imani ya watu katika chombo rasmi cha habari cha Hawza, alisema: Kuchapishwa kwa habari katika Shirika la Habari la Hawza huleta utulivu kwenye jamii ya wanazuoni, kwa sababu wanajua kuwa taarifa zinazotolewa hapo ni sahihi na zenye msingi wa kithibitisho.
Akiwa ni mhusika wa masuala ya utamaduni, alisema pia: Sehemu ya mafanikio ya hivi karibuni katika vyuo vya dini inatokana na juhudi hizi za kitamaduni na za kihabari, na pia kutokana na imani iliyojengeka na uwasilishaji sahihi wa habari. Shughuli za Shirika la Habari la Hawza zina athari kubwa sana.
Afisa Masuala ya Utamaduni na Mtandao wa Kampuni ya Tavanir, akirejelea msisitizo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu juu ya umuhimu wa mtandao, alisema:
Nguvu ya vyombo vya habari ni kubwa kiasi kwamba hata inaathiri wataalamu wa sekta zetu maalumu. Hili linaonesha kwa namna gani simulizi na uundaji wa mtazamo kupitia vyombo vya habari vina ushawishi mkubwa.
Vyombo vya Habari Vinaweza Kubadilisha Uhalisia
Alisisitiza kwa kusema: Sehemu kubwa ya matatizo yanayotukabili leo yanatokana na uzembe katika kazi za kihabari. Historia ya Uislamu nayo haikuokoka na madhara haya; Amirul-Mu’minin (a.s) alikuwa mhanga wa vita vya habari, na Imam Hussein (a.s) pia hali yake ilikuwa hivyo. Jeshi la watu elfu thelathini lililosimama dhidi ya Imam Hussein (a.s) lilikuwa zao la operesheni ya kihabari ya adui wa zama hizo.
Hujjatul-Islam Kakavand, akisisitiza umuhimu wa kazi katika sekta ya vyombo vya habari, alisema: Katika uwanja wa habari, jitihada yoyote inayofanywa ina thamani kubwa. Kila hatua inayochukuliwa kwa ajili ya kuelimisha jamii ni sawa na risasi ambazo Shahidi Haj Qassim Suleimani alikuwa akizielekeza kwa adui. Leo, risasi ya hakika ni vyombo vya habari, ambavyo vinaathiri moja kwa moja akili na nyoyo za wananchi wa nchi yetu.
Vyombo vya Habari: Silaha Madhubuti Katika Vita laini (Soft War)
Afisa Masuala ya Utamaduni na Mtandao wa Kampuni ya Tavanir, akisisitiza kuwa kizazi cha vijana wa miaka ya themanini (kizazi cha sasa cha vijana) endapo kitapata vyombo vya habari vyenye nguvu, kinaweza kila mmoja wao kuwa kama Shahidi Behnam Mohammadi katika uwanja wa jukumu, alisema: Vyombo vya habari vikiwa imara, kizazi hiki kina uwezo mkubwa wa kugeuka kuwa wanajeshi wenye ufahamu, wanaoleta athari chanya kwenye jamii.
Maoni yako