Jumatano 3 Desemba 2025 - 16:14
Ujumbe wa Wanazuoni wa Kishia na Kisunni Kutoka Georgia Watembelea Haram ya Imam Ridha (a.s) Nchini Iran

Hawza/ Ujumbe wa ngazi ya juu ulioongozwa na Rais wa Idara ya Waislamu ya Georgia ulitembelea Haram Tukufu ya Imam Ridha, na pia kushiriki katika programu mbalimbali za kidini na kitamaduni katika hifadhi hii takatifu kwa ukarimu wa uongozi wa Idara ya Wageni wa Haram ya Imam Ridha Wasiokuwa Wairan.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Khorasan, Faek Nabiyev, Rais wa Idara ya Waislamu ya Georgia, jioni ya siku ya Jumanne tarehe 11 ya mwezi wa Azar H.S, akiwaongoza wajumbe 20 wanazuoni na mamuftiy wa Kishia na Kisunni wa nchi hiyo, walifanya ziara katika haram tukufu ya Imam Ridha.

Ujumbe huo uliingia kupitia lango la Shirazi, wakipokelewa na kitengo cha Asia ya Kati cha Idara ya Wageni Wasiokuwa Wairani ya Haram ya Quds Razavi, sambamba na kuandamana na watumishi wa lugha mbalimbali na wabebaji wa ubani, na wakaingizwa chini ya “Mpango wa Ziara ya Ridhwan”.

Ratiba za ujumbe huo zilijumuisha: kuzuru kaburi takatifu la Imam Ridha (a.s), kushiriki Swala ya Jamaa katika Uwanja wa Mtume Mkuu (s.a.w.w), kutembelea Makumbusho ya Qur’ani Tukufu na Maktaba Kuu ya Haram tukufu ya Razavi. Aidha, walikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Haram Tukufu ya Ridha.

Utulivu ni Kitu Kilichopotea kwa Mwanadamu wa Leo

Ridha Khorakiyan, Mkurugenzi Mkuu wa Haram Tukufu ya Ridha, katika kikao hicho akirejea mazingira ya kiroho ya baraza lenye nuru la Ridha alisema: Mafanikio ya kuizuru haram hii tukufu humrudishia mwanadamu wa leo kitu alichokipoteza, yaani utulivu wa moyo.

Msisitizo juu ya Umoja wa Kiislamu na Kuishi Pamoja kwa Dini

Bwana Faek Nabiyev, kiongozi wa ujumbe wa wanazuoni wa Georgia, baada ya ziara yake, kwa kutoa shukrani kwa ukarimu wa ustane Quds Razavi, akirejea mfano halisi wa kuishi kwa amani katika dini mbalimbali nchini Georgia, alisema: Katika mji wa Tbilisi, kuna eneo linaloitwa “Ortajala” ambako ndani yake kuna msikiti wa Mashia, msikiti wa Ahlus-Sunna, kanisa la Orthodox na kanisa la Katoliki yaliyojengwa bega kwa bega, ili kuonesha umoja wa nyoyo za wafuasi wa dini na madhehebu tofauti.

Safari hii ilifanyika kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kitamaduni na kidini kati ya Waislamu wa Georgia, kwa mwaliko wa Majma‘ al-Taqrib Bayna al-Madhahib al-Islamiyyah (Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha