Jumatano 3 Desemba 2025 - 14:14
Palestina Yawasilisha Malalamiko dhidi ya FIFA na UEFA kwa Tuhuma za Kushirikiana Katika Mauaji ya Kimbari

Hawza/ Wanasoka wa Palestina, vilabu vya ndani pamoja na makundi kadhaa ya utetezi wa haki za kimataifa wako katika maandalizi ya kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ambapo wanawashitaki Gianni Infantino, Rais wa FIFA, na Aleksander Čeferin, Rais wa UEFA, kwa tuhuma za kuwezesha miundombinu ya uhalifu na ubaguzi wa Israel.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, licha ya kuonywa mara kwa mara na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na taasisi za haki za binadamu, wawakilishi wa UEFA na FIFA waliwasili katika ardhi zinazokaliwa kimabavu wakiwa na vifaa vyao ili kuendesha mashindano rasmi. Makazi haya ya walowezi yaliyojengwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, kwa mujibu wa sheria za kimataifa na Mikataba ya Geneva, yanatambuliwa kwa mapana kama haramu.

Israel katili, mbali na ukaliaji wake haramu, imetekeleza uhalifu mwingi wa kutisha. Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Habari ya Serikali ya Ghaza, watu 894 kutoka katika jamii ya michezo — wakiwemo wachezaji, waamuzi, makocha na maafisa wa vilabu — wameuawa na Israel, ambapo zaidi ya wanasoka 400 wamo miongoni mwa waliofariki.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, maeneo 292 ya michezo, kuanzia viwanja vya michezo, vilabu, hadi kumbi za mazoezi na maeneo ya wazi yanayotumiwa na wananchi kwa shughuli za michezo, yameharibiwa au kuathiriwa vibaya. Tafiti za kitaaluma zinaonesha pia kulengwa kwa utaratibu miundombinu ya kiraia ya Wapalestina, ikiwemo majengo ya michezo, shule na hata vituo vya afya na matibabu.

Chanzo: Al-Mayadeen

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha