Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Mahmoud Qomati, Makamu wa Rais wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah Lebanon, huku akisisitiza kuwa shambulio la Israel Dhahia kusini mwa Beirut ni ujumbe wa uhasama na ukiukaji wa mamlaka ya Lebanon, alisema kuwa adui haeshimu mkataba wowote.
Akinukuu kwamba kulengwa huko kunawahusu viongozi, wananchi na muqawama, alisisitiza kuwa muqawama baada ya kuthibitisha matokeo ya uvamizi huu, utachunguza jibu mwafaka utakalotoa.
Mahmoud Qomati alisema: “Ujumbe uliotumwa leo na adui wa Kizayuni hukk Dhahia kusini, Hizbullah na Lebanon ni ujumbe mkali na mpya wa uhasama unaothibitisha kuwa adui huyu haeshimu mkataba wowote.”
Mjumbe huyo mwandamizi wa Hizbullah alibainisha kuwa; kulengwa kwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut, ni ujumbe unaoelekezwa kwanza kwa viongozi wa Lebanon—marais watatu, serikali, jeshi, muqawama na wananchi—ukionesha kuwa utawala wa Israel hauheshimu mamlaka wala makubaliano, na unajaribu kuvuka mistari yote myekundu ili kuifanya Lebanon iangukie chini ya matakwa na mradi wa Marekani.
Amesisitiza kuwa baadhi ya viongozi wa Lebanon leo wanaweka matumaini yao katika mazungumzo mapya na adui ambaye hata kifungu kimoja cha makubaliano ya sasa hakutekeleza, na akauliza: “Inawezekanaje kufanya mazungumzo na adui ambaye amekataa kutekeleza hata kifungu kimoja cha makubaliano ya kimataifa yaliyosainiwa chini ya usimamizi wa nchi kubwa, hususan Marekani?”
Qomati ameongeza kuwa; Lebanon leo inahitaji mlingano mpya ambao utawaleta pamoja jeshi, wananchi, serikali na muqawama katika msimamo mmoja, ili kuvunja mlingano ambao adui wa Kizayuni anajaribu kuuweka kwa kupitia uvunjaji kamili wa Lebanon, kwa kudhani kuwa hakuna yeyote anayeweza kumzuia.
Akinukuu kauli ya hivi karibuni ya Netanyahu aliyesema kuwa anaweza kufanya lolote katika Mashariki ya Kati bila kizuizi chochote, Qomati amesisitiza kuwa; hii inaonesha mwendelezo wa uvamizi na ujeuri.
Qomati ameeleza kuwa; muqawama baada ya kuthibitisha matokeo ya uvamizi huu utaangalia na kuchukua uamuzi muafaka.
Maoni yako