Jumanne 18 Novemba 2025 - 17:16
Muungano wa Muqawam kutoka Palestina hadi Caracas na Havana; Jiografia Tatu dhidi ya Ubeberu wa Magharibi

Hawza/ Katika mazingira ambayo vita, vikwazo na mzingiro vimekuwa nyenzo endelevu za nguvu za mataifa ya Magharibi, mataifa matatu—Palestina, Venezuela na Cuba—pamoja na umbali wa kijiografia baina yao, yamekuwa mhimili wa pamoja wa muqawama, kujitafutia uhuru na kutetea amani ya haki. Mataifa haya matatu ambayo kwa miaka mingi yamekuwa chini ya shinikizo la mifumo ya kiimla, leo ni alama ya kusimama imara kwa upande wa Kusini wa Dunia dhidi ya utaratibu usio wa haki wa kimataifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, mabadiliko ya miaka ya hivi karibuni yanaonesha kwamba; muundo wa nguvu za Magharibi upo katika mgogoro mkubwa zaidi katika miongo kadhaa. Uanzishaji wa vita, vikwazo vinavyodhoofisha na uvamizi wa kijeshi na kiandishi, vimekuwa sera za kawaida za serikali za Marekani na Ulaya, na zimeweka usalama wa dunia mikononi mwa malengo ya kijiopolitiki ya mataifa makubwa.

Kuanzia kukaribia kwa manuwari za Marekani kwenye maji ya Venezuela kwa kisingizio cha “kupambana na dawa za kulevya” hadi kuunga mkono mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza bila masharti, na pia kuendelea kwa mzingiro wa kiuchumi dhidi ya Cuba, vyote hivi ni dalili za ubeberu wa kisiasa na kijeshi unaozuia amani ya kudumu duniani.

Venezuela chini ya shinikizo la vita mseto

Miezi ya karibuni kumekuwa na ongezeko la shinikizo la kiuchumi, uandishi na kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Bolivaria ya Venezuela. Vikwazo vipya, operesheni za kisaikolojia na juhudi za kuimarisha viongozi wanaotengenezwa na Magharibi kwa lengo la kusababisha kuyumba kwa hali ya ndani ni sehemu ya mkakati wa Washington dhidi ya Caracas.

Licha ya vitisho hivi, Venezuela, kwa kutegemea sheria za kimataifa na msaada wa washirika wa eneo, imesimama katika kutetea mamlaka ya kitaifa. Wachambuzi wanaona Venezuela ya leo kama mwendelezo wa fikra ya kujitafutia uhuru ya Amerika ya Kusini—fikra ambayo imeanzia Bolivar hadi Hugo Chavez.

Palestina na Cuba; sura za kihistoria za muqawa

Huko Palestina, mashambulizi endelevu ya utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo ya makazi ni ukiukaji wa wazi wa haki za kibinadamu na sheria za kimataifa. Licha ya hilo, msaada wa kisiasa na kijeshi wa Magharibi kwa Tel Aviv unaendelea. Mapambano ya Wapalestina dhidi ya uvamizi siyo tu vita kwa ajili ya ardhi; bali ni kupambana na mantiki ya ukoloni, ubaguzi wa rangi na utawala wa kijeshi.

Nchini Cuba, zaidi ya miaka sitini ya mzingiro wa kiuchumi haijafanikiwa kuizuia nchi hii katika njia yake ya kujitegemea na kutafuta haki. Mfano wa Cuba katika sekta kama afya na elimu bado ni ishara ya kusimama imara dhidi ya shinikizo la kimfumo kutoka Magharibi.

Mizizi ya kihistoria; kutoka Bandung hadi harakati za Kusini wa Dunia

Mwelekeo wa mapambano katika jiografia hizi tatu una uhusiano wa kina na historia ya kujitawala kwa mataifa. Kuanzia Mkutano wa Bandung mwaka 1955 hadi kuundwa kwa Harakati ya Kutokutumia upande wowote, pamoja na wimbi jipya la ushirikiano wa Kusini mwa Dunia, mawazo kama “haki ya kujitawala” na “kuishi kwa amani” yameunda msingi wa fikra ya mwelekeo huu.

Kanuni tano kuu za kuishi kwa amani—heshima ya pande zote, kutovamia, kutokuingilia mambo ya ndani, usawa na maslahi ya pamoja—leo hii zinajidhihirisha kwa namna kubwa katika sera za nchi kama China, Venezuela, Iran, Afrika Kusini na Cuba.

Mtandao wa Kutetea Ubinadamu; mshikamano wa kimataifa wa muqawama

Mtandao wa “Kutetea Ubinadamu” unaoongozwa na Cuba, umegeuka kuwa jukwaa la kuunganisha wanazuoni, wasanii na wanaharakati wanaotetea amani dhidi ya vita vya kiandishi na mzingiro wa kiuchumi. Mtandao huu unaimarisha simulizi la mapambano ya mataifa dhidi ya ubeberu katika kiwango cha kimataifa, na kusisitiza uhusiano kati ya utamaduni, kujitafutia uhuru na amani.

Mataifa ndiyo waandishi wa historia

Leo hii tuko mbele ya picha mbili kinzani za dunia: dunia inayotegemea vikwazo, vita na kulazimisha matakwa ya mataifa makubwa, na dunia inayotegemea heshima, ushirikiano na kuishi kwa amani.

Kotoka Ghaza hadi Caracas, na kutoka Havana hadi maeneo mengine ya Kusini wa Dunia, mataifa yamethibitisha kwamba; mshikamano na irada ya pamoja vinaweza kubadilisha mkondo wa historia—kama ilivyo katika kauli mbiu ya kihistoria ya wapiganaji: Popote taifa linaposimama, mataifa yote yanapiga hatua mbele.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha