Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, matokeo na tathmini za uchaguzi wa Iraq yanaonesha dalili za kurejea tena kwa ubora wa upande wa Muqawama mbele ya makundi ya kiliberali na waliokaribu na fikra za Baath waliopungua kwa kiasi kikubwa katika kura. Ushindi wa makundi kama Badr, Huquq, Qanun na al-Sadiqun unaonesha kuwa wananchi wa Iraq wamepiga kura ya kuendelea kuwepo kwa jeshi la muqawama katika kulinda uhuru wa nchi. Muundo mpya wa bunge utakuwa kizuizi kikubwa dhidi ya mipango ya Marekani ya kudhoofisha Hashd al-Sha’abi.
Muhammad Sadiq al-Hashimi, mwandishi wa Kiiraq na Mkurugenzi wa Kituo cha Tafiti za Iraq, pamoja na kuchambua matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini humo, aliandika:
“Mtu yeyote anayefuatilia vyombo vya habari vya Magharibi, ikiwemo magazeti yote, makala na tafiti za magazeti ya nje na ya Kiarabu, ataingia katika mshangao mkubwa. Machapisho haya yanaonesha kwa njia mbalimbali kwamba ushindi uliopatikana Iraq ni ushindi wa muqawama, wa Marjaiyyah ya dini na wa Iran.”
Katika muktadha huo, ninaelezea mambo yafuatayo:
Ushindi uliopatikana Iraq, kwa ushiriki mpana wa wananchi, unaonesha waziwazi nafasi ya Najaf na Iran, na ni ushahidi kwamba ushindi mkubwa wa Waislamu wa Kishia na mhimili wao wa karibu ni ushindi wa muqawama na kurejea kwa utamaduni wa wilaya.
Iran, baada ya matukio ya "Tofanu’l-Aqsa", imerejea kwa nguvu katika kupanga masuala ya Waislamu wa Kishia wa eneo, na kwa sasa inashughulikia makosa na kuzuia vurugu ambazo adui alikuwa akipanga — moja ya matokeo ya vita ya Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mhimili wa muqawama — ili Waislamu wa Kishia wasipoteze nafasi yao muhimu katika serikali ya Iraq na eneo.
Matokeo haya na ushindi wa Waislamu wa Kishia yamedhihirisha kuwa Iran ina tajriba na mbinu tofauti za kuwaamsha wananchi wa Iraq, kuwahamasisha, kuwawekea utaratibu, kuendeshea mchakato wao wa kisiasa, na kuipulizia roho ya uhai, matumaini, muqawama na uthabiti wa kisiasa katika utamaduni na harakati za watu wa Iraq.
Ushiriki mpana na matokeo yaliyopatikana ni ushindi mkubwa kwa Najaf, Iran na mhimili wa muqawama. Kama Wamarekani na Wazayuni walivyoshindwa kijeshi wakati wa vita vya Tofanu’l-Aqsa, vivyo hivyo wameshindwa katika uwanja wa kisiasa. Na huu ni ukweli.
Iran bado inadhibiti mafaili muhimu ya eneo na ina uwezo wa kuathiri. Matukio yaliyotokea katika eneo hayajaitenga Iran na ushawishi wake katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu wala katika muqawama. Kwa ushindi wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq, Iran imeweza kusema kwamba imefanikiwa kuhuisha nguvu ya Waislamu wa Kishia na mhimili wa muqawama.
Iran na mhimili wa muqawama wako katika hatua ya kuhamia kutoka katika mtazamo wa upande mmoja wa muqawama wa kijeshi kuelekea katika sura pana ya kisiasa kupitia ushiriki mpana wa makundi ya Kishia yaliyo karibu nao. Ushindi huu, kwa hakika, umeongeza ushindi wa Waislamu wa Kishia.
Salamu ziwe juu ya Waislamu wa Kishia wa Iraq, viongozi wao wa dini na damu yao safi.
Maoni yako