Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, mijumuisho ya mijadala ya Mahdawiyya ikiwa na anuani isemayi “Kuielekea Jamii Bora”, ikiwa na lengo la kusambaza mafundisho na maarifa yanayohusiana na Imam Mahdi (a.t.f.s), tunakufikishieni nyinyi waheshimiwa na wasomi.
Lengo la uumbaji ni kumuadu Mwenyezi Mungu Mtukufu¹, na msingi wa kufanya ibada ni kumjua Yeye². Dhihirisho la juu kabisa la maarifa haya ni kumjua Mtume (s.a.w.w) na wasii wake. Bila shaka, mojawapo ya majukumu muhimu ya waja mbele ya Mola wao ni kumjua huyo Mwenye utakasho wa Kiungu. Maarifa haya hufikia ukamilifu pale Mitume wa Mungu – hasa Mtume wa Mwisho (s.a.w.w) – wanapojulikana vyema. Jambo hili pia halitapatikana ila kwa kuwajua wasii wake, haswa Hujjah wake wa mwisho.
Mtu mmoja alimuuliza Imam Hussein (a.s.):
«یَا اِبْنَ رَسُولِ اَللَّهِ بِأَبِی أَنْتَ وَ أُمِّی فَمَا مَعْرِفَةُ اَللَّهِ قَالَ مَعْرِفَةُ أَهْلِ کُلِّ زَمَانٍ إِمَامَهُمُ اَلَّذِی یَجِبُ عَلَیْهِمْ طَاعَتُهُ.»
“Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu! Baba na mama yangu wawe fidia kwako! Nini maana ya kumjua Mwenyezi Mungu?” Imam Hussein (a.s.) akajibu:
“Kumjua Mwenyezi Mungu ni kwamba watu wa kila zama wamtambue Imam wao ambae kumtii yeye ni wajib juu yao.”
(‘Ilal al-Sharāyi‘, Juzuu ya 1, uk. 9)
Hivyo basi, kumjua Imam hakutengani na kumjua Mwenyezi Mungu, bali ni miongoni mwa vipengele vyake.
Katika dua iliyo pokewa kutoka kwa upande mtukufu (wa Imam Mahdi) imesemwa:
«اللَّهُمَّ عَرِّفْنِی نَفْسَکَ فَإِنَّکَ إِنْ لَمْ تُعَرِّفْنِی نَفْسَکَ لَمْ أَعْرِفْ نَبِیکَ، اللَّهُمَّ عَرِّفْنِی رَسُولَکَ فَإِنَّکَ إِنْ لَمْ تُعَرِّفْنِی رَسُولَکَ لَمْ أَعْرِفْ حجّتکَ، اللَّهُمَّ عَرِّفْنِی حجّتکَ فَإِنَّکَ إِنْ لَمْ تُعَرِّفْنِی حجَّتَکَ ضَلَلْتُ عَنْ دِینِی.»
“Ee Mola! Nifahamishe mimi dhati yaki, kwani kama Hutanijulisha dhati yaki, sitamjua Mtume wako.
Ee Mola! Nijulishe mimi Mtume wako, kwani kama Hutonijulisha Mtume wako, sitamjua Hujjah wako. Ee Mola! Nijulishe mimi Hujjah wako, kwani kama Hutonijulisha Hujjat wako, nitapotea kuepukana na dini yangu.”
(al-Kāfī, Juzuu ya 1, uk. 342)
Njia Kuu Tatu za Kumtambua Imam
1. Nass (Nass ya Kuteuliwa)
Nass maana yake ni kutajwa wazi na Mtume (s.a.w.w) kuhusu Imam fulani, ambayo maana yake ni habari ya uteuzi wa Kiungu au uteuzi wa Imam kwa amri ya Mwenyezi Mungu.
Aina ya kwanza: Uteuzi unaotoka moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu, na Mtume anautangaza tu.
Aina ya pili: Uteuzi unatokea kwa kupitia Mtume kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na kuutegemeza huo kwake ni kama kutengemeza vitendo vya Malaika kwa Mwenyezi Mungu.
2. Karama
Kutokea kwa karama mikononi mwa mwenye kudai Uimamu ni dalili ya ukweli wa madai yake, na kwa baadhi ya wanazuoni, ni dalili ya kwamba ameteuliwa na Mwenyezi Mungu.
Kuna mitazamo miwili:
Mosi. Karama ni dalili huru ya Uimamu.
Pili. Dalili kuu ni nassi ya Mtume au Imam aliyemtangulia; karama ni uthibitisho wa uwepo wa nassi hiyo, hata kama haikufika kwetu.
3. Sira ya Kiutendaji (Mfumo wa Maisha na Tabia)
Akhlaki, mwenendo, elimu, hekima, maneno na misimamo ya mtu ni njia ya kumtambua Imam kwa wale wenye uwezo wa kutambua alama za Uimamu.
(Rejea: Lutfullah Safi Golpaygani, “Piramuni Ma‘rifat al-Imam”, uk. 77–78)
Leo hii kuna Riwaya yofauti zinazo muelezea Imam Zama (aj), Imam wa nane kwa Mashia, Imam Ridhaa (a.s.) anasema kuhusu Sifa za Imam:
«... الاِمَامُ أَمِینُ اللَّهِ فی خَلْقِهِ، وَحُجَّتُهُ، عَلَی عِبَادِهِ، وَخَلِیفَتُهُ فِی بِلادِهِ، وَالدَّاعِی إِلَی اللَّهِ، وَالذَّابُّ عَنْ حُرَمِ اللَّهِ، الاِمَامُ الْمُطَهَّرُ مِنَ الذُّنُوبِ، وَالْمُبَرَّأُ عَنِ الْعُیُوبِ، الْمَخْصُوصُ بِالْعِلْمِ، الْمَوْسُومُ بِالْحِلْمِ نِظَامُ الدِّینِ، وعِزُّ الْمُسْلِمِینَ، وَغَیْظُ الْمُنَافِقِینَ، وَبَوَارُ الْکَافِرِینَ، الاِمَامُ وَاحِدُ دَهْرِهِ لا یُدَانِیهِ أَحَدٌ، وَلا یُعَادِلُهُ عَالِمٌ، وَلا یُوجَدُ مِنْهُ بَدَلٌ، وَلا لَهُ مِثْلٌ وَ لا نَظِیرٌ، مَخْصُوصٌ بِالْفَضْلِ کُلِّهِ مِنْ غَیْرِ طَلَبٍ مِنْهُ لَهُ وَلا اکْتِسَابٍ، بَلِ اخْتِصَاصٌ مِنَ الْمُفْضِلِ الْوَهَّابِ ...»
“Imam ni mwaminifu wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa viumbe wake; ni Hujjat yake juu ya waja wake; ni khalifa wake katika ardhi zake; ni mlinganizi wa watu kumuelekea Mwenyezi Mungu; ni mtetezi wa mipaka ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake.
Imam ni mtoharifu kutokana na dhambi; ni mwenye kuepushwa na upungufu; elimu imetengwa kwake; anafahamika kwa upole; ni mpangiliaji wa dini; ni utukufu wa Waislamu; ni ghadhabu ya wanafiki; ni maangamizi kwa makafiri.
Imam ni wa kipekee katika zama zake, hakuna anayeweza kusogea karibu na daraja lake, wala mwanazuoni yeyote hafanani naye, wala hapatiwi badala, wala hana mfano au kifananishi.
Fadhila zote zimetengwa kwake, bila yeye kuziomba au kuzitafuta – ni uteuzi kutoka kwa Mwenye Kutoa neema, Mkarimu Mwenye Kutoa bila kipimo.”(al-Kāfī, Juzuu ya 1, uk. 201)
Utafiti huu unaendelea…
Imenukuliwa kutoka katika kitabu “Darsnāme-ye Mahdawiyyat” kilichoandikwa na Khudāmarād Salimiyān, huku ikifanyiwa mabadiliko madogo.
Rejea:
1. “Wama khalaqtul-jinna wal-insa illa liya‘budūn” – “Sikumuumba majini na watu ila waniabudu.” (Dhāriyāt 51:56)
2. “Awalu ‘ibādatillāh ma‘rifatuhu” – “Ibada ya kwanza ya Mwenyezi Mungu ni kumjua Yeye.”
(Rejea: Shaykh al-Sadūq, Tawhīd, uk. 34; Shaykh al-Tūsī, Amālī, uk. 22)
Maoni yako