Jumanne 18 Novemba 2025 - 17:33
Wajibu wetu wa kitaifa na wa kisheria unatiwajibisha kuitetea ardhi yetu

Hawza/ Ali Kharis, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Amal na mwakilishi wa Bunge la Lebanon, amesisitiza kuwa uchaguzi wa bunge utafanyika kwa mujibu wa sheria iliyopo na katika muda uliopangwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ali Kharis, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Amal na mwakilishi wa Bunge la Lebanon, katika hafla ya kukumbuka mwaka wa kwanza tangia kupata shahada ya Ali Kamal Suleiman, iliyoandaliwa na Harakati ya Amal katika mji wa al-Bayadh, alisisitiza kwamba uchaguzi wa bunge utafanyika kwa mujibu wa sheria ya sasa na katika wakati wake uliopangwa; na kwamba yeyote anayetafuta marekebisho au kupendekeza mswada, kwa hakika shabaha yake ni kuahirisha uchaguzi.

Akasema: “Msimamo wa Harakati ya Amal uko wazi na wa moja kwa moja, na hakuna nafasi ya mabadiliko yoyote au ucheleweshaji.”

Mjumbe huyo wa Harakati ya Amal aliwatumia salamu za heshima mashahidi wote walioutoa uhai wao kwa ajili ya kuendelea kuwapo kwa Lebanon, na akatoa ahadi kwa wote kwamba watabaki juu ya njia hiyo hiyo na mkataba huo huo.

Aidha, alitoa shukrani kwa juhudi za Jumuiya ya jeshi la ulinzi wa raia, ambao walikuwepo uwanjani kuanzia Naqoura hadi Shebaa, wakijitoa muhanga na kutekeleza wajibu wao kwa njia bora kabisa.

Kharis alisema: “Tupo katika hatua ngumu, na adui Muisraeli kila siku hututishia kwa mabomu, mauaji na uharibifu, naye anapata uungwaji mkono wa kimataifa na Marekani. Cha kusikitisha ni kwamba ndani ya nchi pia wapo watu ambao, kwa misimamo na matamshi yao, wanamuunga mkono adui na wanamhamasisha adui Muisraeli kuendelea na anachokifanya; jambo ambalo linaathiri umoja wa kitaifa.”

Mwakilishi huyo wa Bunge la Lebanon aliendelea kusema: “Kukabiliana na adui hakuwezekani isipokuwa kwa umoja, mshikamano na kuishi kwa amani baina yetu, kwani taifa hili ni taifa la mwisho kwa watoto wake wote. Wote kwa pamoja tunalazimika kushirikiana kulilinda na kulitetea, mbali na njama zinazoandaliwa dhidi ya viongozi na watu wenye hadhi ya kitaifa.”

Mwisho, alisema: “Wajibu wetu wa kitaifa na wa kisheria unatuwajibisha kulitetea taifa letu, mipaka yetu, nchi yetu, kusini kwetu na watu wetu, kwa gharama yoyote ile, hata kama kunahitaji kujitoa muhanga na kufa kishahidi.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha