Jumanne 11 Novemba 2025 - 23:25
Tafsiri ya Qur’ani Tukufu kwa Lugha ya Rohingya

Hawza/ Tafsiri ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Rohingya imekuwa ikijadiliwa kwa miaka mingi kwa lengo la kufufua utambulisho wa kidini na Kiislamu wa Waislamu wa Myanmar, lakini kila mara juhudi hizo zimekabiliwa na ukandamizaji kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, kwa muda wa zaidi ya miaka kumi, Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakikumbana na mateso makali kutoka kwa serikali ya Myanmar. Tangia mwaka 2014 hadi sasa, zaidi ya watu 740,000 wamelazimika kukimbilia nchini Bangladesh baada ya vijiji vyao kuchomwa moto.

Lugha ya Rohingya ni lugha yenye asili ya Indo-Aryan, ambayo kwa miongo mingi imebakia katika mfumo wa mazungumzo pekee bila maandishi. Hata hivyo, kutokana na juhudi za mwanazuoni maarufu Muhammad Hanif, mfumo wa maandishi ujulikanao kama “Herufi ya Hanifi” ulianzishwa mwaka 2018 kwa ajili ya kuandika lugha ya Rohingya. Kupitia juhudi hizo, lugha hiyo imeweza kujumuishwa katika orodha ya lugha za kimataifa zilizo na viwango rasmi.

Mradi wa kutafsiri Qur’ani ulianza kwa tafsiri za kusikiliza na kutazama (audio-visual) ili kuwafikia wale wasiofahamu kusoma na kuandika. Baadaye, toleo la maandishi lililotumia herufi ya Hanifi likatayarishwa, ambapo tafsiri ya sura tano za mwanzo za Qur’ani imekamilika. Inapangwa kwamba nakala 2000 za tafsiri hiyo zichapishwe na kusambazwa katika nchi za Saudia, Malaysia, na Bangladesh.

Chanzo: Shia Waves Agency

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha