Jumapili 9 Novemba 2025 - 10:20
Hitimisho la shughuli za siku ya kwanza za Mkutano wa Nne Kimataifa wa Elimu “Dar Al-Rasul Al-A‘zam (sa.w.w)” 

Hawza/ Haram takatifu la Abbasi, imekamilisha shughuli za siku ya kwanza za Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa Elimu «Dar Al-Rasul Al-A‘zam (s.a.w.w).

Kwa Mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Haram takatifu ya Abbasi imekamilisha shughuli za siku ya kwanza za Mkutano wa Kimataifa wa Elimu «Dar Al-Rasul Al-A‘zam (saww).

Mkutano huu umeandaliwa na Idara ya Masuala ya Fikra na Utamaduni katika Haram takatifu ya Abbasi, kwa ushirikiano na Chuo cha Mafunzo ya Awali kwa Wasichana katika Chuo Kikuu cha Al-Ameed, ukiwa na maudhui isemayo: “Sira tukufu ya Mtume kati ya Misingi ya Qur’ani na Mabadiliko ya Kielimu”. Shughuli zake zitaendelea kwa siku mbili.

Shughuli za siku ya kwanza zilijumuisha: onyesho la filamu lililokuwa likiwasilisha mkutano na programu zake, pamoja na kuandaliwa kwa vikao vitatu vya utafiti ambavyo vilihusisha washiriki 19 kutoka ndani na nje ya Iraq, ambapo walijadili na kuchambua baadhi ya makala za kielimu. Aidha, washiriki wa programu za mkutano waliheshimiwa kwa mchango wao.

Mkutano huu ulikuwa na ushiriki wa watafiti kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu na Kiislamu, pamoja na watafiti wa vyuo vikuu vya Iraq. Ushiriki wa kimataifa ulijumuisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Uturuki, Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Aljeria, Tunisia, Lebanon, Pakistan na Moroko.

Lengo la mkutano ni kuangazia sira takatifu ya Mtume (saww) kama mfano wa kiutu na mbinu ya kielimu inayokubalika, na kuionyesha katika mwanga wa misingi ya Qur’ani na mabadiliko ya fikra za kisasa katika mbinu za utafiti wa kielimu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha