Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kundi la wanazuoni wa Lebanon lilikutana na kufanya mazungumzo na Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Vyuo vya Dini vya Kiislamu vya Iran, pembezoni mwa kongamano la kimataifa la kumbukumbu ya Allāmah Mirzā Nainī.
Sheikh Hussein Qubris, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Muqāwama, akizungumza katika kikao hicho, alionesha furaha yake kwa kukutana na Ayatullah A‘rafi na kupongeza uandalizi wa kongamano hilo muhimu.
Alitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano wa kielimu na kitamaduni, pamoja na kutambulishwa zaidi kwa mashahidi wa harakati ya muqāwama wa Lebanon, akiwemo Sayyid Abbas Musawi, Sayyid Hassan Nasrullah, na wanazuoni mashahidi wa harakati hiyo.
Akasema: “Leo hii, ni jambo lenye umuhimu mkubwa kuwawatambulisha wanazuoni na watu wenye athari katika ulimwengu wa Kiislamu. Kuwatambulisha watu kama Mirzā Nainī na wanazuoni wa zama hizi kunachangia kuwafanya watu na wanafunzi wa dini waufahamu zaidi fikra na misingi ya hawa wakubwa.”
Kisha akaongeza kusema: “Utawala wa Kizayuni unajaribu kubadilisha hesabu za kisiasa katika eneo hili kwa maslahi yake, lakini mhimili wa muqāwama umesimama imara kwa nguvu na azma. Hizbullah leo ni imara zaidi kuliko wakati wowote, na njama za maadui za kuivuaa silaha Hizbullah na Hamas zitashindwa.”
Kwa upande wake, Ayatullah A‘rafi aliwakaribisha wageni kwenye kongamano hilo, na akaeleza kwa ufafanuzi kuhusiana na vyuo vya dini vya Iran, huduma, mafanikio ya kielimu, kimasomo, kiutume na kitamaduni, pamoja na shughuli zake za kimataifa.
Akaelezea pia nyanja za kifikra, kisiasa na kielimu za Allāmah Mirzā Nainī, akisisitiza juu ya umakini na uangalifu wa mwanazuoni huyo jihadi katika kufuatilia hali za zama zake.
Akasema:
“Nafasi yake katika kupambana na ukoloni wa Kiingereza, kutetea uhuru wa jamii ya Kiislamu dhidi ya wakoloni, na katika kuunda msingi wa serikali ya Kiislamu, ilikuwa ya umuhimu mkubwa.”
Mjumbe wa Baraza Kuu la hawza aliongeza kusema: “Katika zama za Allāmah Mirzā Nainī (r.a), kulikuwa na mageuzi makubwa ya kisiasa na kijamii katika ulimwengu wa Kiislamu. Yeye, kwa uchambuzi wa kina wa hali halisi na kwa ufahamu wa mazingira ya wakati wake, aliweza kuchukua misimamo yenye uwazi na mikakati madhubuti iliyobeba upeo wa kielimu, kifiqhi, kisiasa na kijamii.”
Maoni yako