Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh al-Qattan aliyasema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa kitaifa wa Lebanoni–Palestina uliofanyika katika mgahawa wa al-Sāha, kufuatia mwaliko wa harakati ya Hamas, amesema:
“Baada ya yote tuliyoyaona Palestina, hasa huko Ghaza na Lebanon, tunapaswa kuwaenzi mashujaa waliopigana jihadi na wale waliouawa kishahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakiitetea heshima na izza ya umma huu. Tunatoa shukrani zetu kwa wote walioiunga mkono Ghaza na Palestina na kusimama imara pamoja nao.”
Akaendelea kusema: “Tunawashukuru watu wa Gaza kwa subira yao na uthabiti wao, na tunawashukuru watu wa Lebanon na Yemen kwa kusimama bega kwa bega na Ghaza, pamoja na wote walioiunga mkono Palestina. Lebanon imetoa watu na viongozi wake bora; kiongozi wa mapambano ya Kiislamu Lebanon alijitolea nafsi yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, akasimama imara katika kuilinda Ghaza, na akaunga mkono ulinzi wa Ghaza kwa Lebanon na Yemen tukufu.”
Sheikh al-Qattan akaongeza kwa kusisitiza: “Tumeona namna alivyokuwa tayari kujitolea kwa dhati katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kuitetea Ghaza. Kwa hivyo, tunapaswa kurekebisha dira zetu, na kuyaamsha mataifa ya Kiarabu na Kiislamu ili yatambue thamani na hadhi ya wale wakubwa wetu waliotoa maisha yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”
Maoni yako