Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ofisi ya Marja‘ mwenye heshima kubwa, Mtukufu Ayatullah Sayyid Ali Husayni Sistani mjini Najaf Ashraf, imetoa taarifa ikieleza kwamba leo, Alhamisi, itakuwa siku ya mwisho ya mwezi wa Rabi‘ al-Thani, na Ijumaa, tarehe 24 Oktoba 2025, itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Jumada al-Ula mwaka 1447 Hijria Qamariyya.
Inafaa kutajwa kuwa Kamati ya Kuchunguza Mwandamo wa Mwezi ya Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Mtukufu Ayatullah Khamenei, jioni ya jana Jumatano (29 Rabi‘ al-Thani 1447), imetangaza kwamba hilali ya mwezi ulimeonekana katika baadhi ya maeneo ya nchi kwa kutumia vifaa vinavyo saidi uono.
Maoni yako