Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ali Fayyadh, mwakilishi wa Bunge la Lebanon, katika hotuba yake kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya shahada ya Sheikh Nabil Qawuq, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Utekelezaji la Hizbullah, na mashahidi wa mji wa kusini wa Abba — tukio lililohudhuriwa na viongozi na familia za mashahidi — alisema: Imebainika kuwa baadhi ya watu walioko madarakani wanatekeleza kwa makusudi siasa ya kutekeleza kila kipengele kinacholeta mvutano na uchochezi ndani ya nchi, na wanazidisha tofauti na migawanyiko, wakifanya hivyo kwa lengo la kuitenga kabisa jjamii; jambo ambalo ni uvunjaji hatari wa kanuni za Mkataba unaounda msingi wa uthabiti wa ndani wa taifa.
Fayyad aliongeza: Baadhi ya maafisa wanafanya kana kwamba katika uhusiano wao na nguvu za kigeni ni “wafalme kuliko mfalme mwenyewe”, na wananguvu kuliko mipaka yote ya kisheria.
Alisema kwamba: Yule ambaye anapaswa kuwa mlinzi wa haki, sheria na stahiki za Walebanon, ameyageuza maadili hayo kuwa zana za kisiasa kwa ajili ya kulipiza kisasi na kutafuta ridhaa za nguvu za kigeni, kwa visingizio visivyomshawishi yeyote na ambavyo havina ulazima wowote wa kitaifa.
Mwakilishi huyo wa Bunge la Lebanon alisema: Iwapo mwenendo huu utaendelea katika mwelekeo wake wa kisheria wa sasa, utasababisha sehemu kubwa ya wananchi wa Lebanon kubadilika kuwa kundi lililopuuzwa, lisilo na haki wala mustakabali. Itatosha tu Wamarekani wamjumuishie kiholela na bila haki raia yeyote katika orodha zao, kisha maafisa wa Lebanon wapitishe hukumu ya kisheria na kiuchumi dhidi yake, huku wakimnyima haki ya kumiliki, kufanya kazi, au hata kujipatia riziki halali.
Fayyadh alisisitiza kwamba: Mwenendo huu unaonyesha tabia ya kiuchokozi yenye misingi ya kisiasa ambayo haiendani na maslahi ya wananchi, bali inaleta matokeo mazito ya kisiasa na kijamii.
Mwisho, alisisitiza kuwa mwenendo wa baadhi ya watu walioko madarakani umekuwa chanzo chenye kuketa wasiwasi na hasira kwenye ngazi za juu kabisa, na hali hiyo haiwezi kuelezewa tu kama uzembe au udhaifu wa maamuzi, bali ni jaribio la makusudi la kuchochea migogoro ya ndani hadi kilele chake na kuitumbukiza nchi katika hatua mpya na hatari
Maoni yako