Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hussein Kuhsari, Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza za Kielimu, alisafiri kuelekea Lebanon kwa lengo la kukuza mahusiano ya kielimu na kitamaduni. Alianza ratiba yake kwa kushiriki katika shughuli za eneo la Bekaa na mji wa kihistoria wa Baalbek.
Katika ziara hii, pamoja na kutoa heshima kwa nafasi tukufu ya Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon, Shahidi Sayyid Abbas Musawi, Kuhsari alifanya mikutano muhimu na familia za mashahidi, maulamaa na wakurugenzi wa Hawza za eneo hilo, na kusisitiza nafasi ya msingi ya Muqawama na fikra za Mapinduzi ya Kiislamu.
Shughuli ya kwanza ya Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza ilikuwa ni kutembelea kaburi la Shahidi Sayyid Abbas Musawi, Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon. Hujjatul-Islam Kuhsari, kwa kutoa heshima kwa shahidi huyu mkubwa, alikumbuka kwa taadhima kumbukumbu zake. Baada ya hapo, alikutana na familia tukufu ya Shahidi Musawi pamoja na kundi la maulamaa na wanazuoni mashuhuri wa eneo hilo kwa ajili ya mazungumzo.
Baadaye, Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza alielekea katika Hawza ya Imam al-Muntadhar (aj) inayosimamiwa na Ayatullah Sayyid Muhammad Yazbek. Akiwa huko, alifanya kikao cha pamoja na Ayatullah Yazbek, mwanawe, wakurugenzi na walimu wa kituo hicho cha kielimu. Pia, katika mazingira ya urafiki na ukaribu, alizungumza na wanafunzi vijana wa Hawza hiyo.
Maoni yako