Jumanne 30 Septemba 2025 - 06:38
Ujumbe wa rambirambi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Iran, kwa Ayatollah al-Uzma Sistani

Hawza/ Mtukufu Ayatollah Khamenei katika ujumbe wake ametoa rambirambi kufuatia kufariki kwa mke mtukufu wa Ayatollah Sistani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

Mtukufu Ayatollah Sayyid Ali Sistani (Allah adumishe baraka zake),

Ninatoa mkono wa rambirambi kufuatia kufariki kwa mke wake mtukufu, na ninamuombea kwa Mwenyezi Mungu rehema na msamaha.

Sayyid Ali Khamenei
29 September 2025

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha