Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, wataalamu wa Umoja wa Mataifa baada ya kuthibitisha mauaji ya halaiki ya Israel huko Ghaza, wamezitaka timu za Israel zisitishe kushiriki katika michezo na wamesema: “Wakati umefika wa kufutilia mbali fikra kwamba mpira wa miguu ni biashara.”
Mwezi Agosti, katika mchezo wa Super Cup kati ya Paris Saint Germain na Tottenham, watazamaji na wanachama wa UEFA walibeba mabango yenye ujumbe: “Acheni kuua watoto; acheni mauaji ya raia wasio na hatia.”
Kabla ya hapo, Marekani katika dai la kifedhuli ilikuwa imesema kwamba kwa kuwa Kombe la Dunia lijalo la 2026 litafanyika pia nchini humo, iwapo FIFA itatishia Israel, Marekani itaingilia kati, hata ufidheli huo ulifikia kiwango kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, katika mahojiano na Sky News, alisema: “Tutaizuia FIFA isiisimamishie Israel kushiriki Kombe la Dunia.”
Israel tangia kuanza kwa mauaji yake ya halaiki imeua zaidi ya Wapalestina 65,000, wakiwemo mamia ya wanamichezo na maelfu ya watoto na raia wasio na hatia.
Chanzo: MIDDLE EAST EYE
Maoni yako