Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, kwenye maandamano makubwa nchini Italia wananchi waliukosoa vikali ushirikiano na usaidizi wa serikali ya Italia kwa utawala katili na jinai wa Israel.
Wandamanaji pia walipaza sauti zao kuunga mkono meli na manowari zote zinazojitahidi kuvunja mzingiro wa Ghaza, katika maandamano hayo, baadhi ya vyama vya wafanyakazi vilitangaza kuendelea mgomo hadi pale serikali itakapositisha msaada na ushirikiano wake na utawala wa Kizayuni, miongoni mwao ni Muungano wa Wafanyakazi Huru na Muungano wa Kitaifa wa Wafanyakazi wa Italia.
Guido Lotrio, katibu wa Muungano wa Kitaifa, alisema: “Lengo la mgomo wetu ni kuishinikiza serikali ichukue hatua madhubuti zaidi dhidi ya Israel muhalifu, Iwapo serikali haitazingatia matakwa ya wananchi, tutazidisha shinikizo — tutafunga bandari na vituo, na kuzuia kila aina ya biashara ili kuifanya serikali ishindwe kufanya kazi, ni bora waache usaidizi wa kifedha na ushirikiano na Israel kabla hali haijawa ngumu zaidi.”
“Sisi ndio wananchi wa Italia; tunataka kusimama upande sahihi wa historia, tarehe 18 Septemba tulizuia meli mbili zilizokuwa na shehena ya vilipuzi vilivyokuwa vinapelekwa Israel kupitia ripoti na jitihada zetu, lakini bado serikali haijaacha ushirikiano wake na utawala wa Kizayuni,” aliongeza.
Ricardo Rudino naye alisema katika mahojiano: “Iwapo tutapoteza mawasiliano na meli zinazokwenda Ghaza au zikishambuliwa, naahidi mara moja kufunga bandari zote za Ulaya mpaka uchumi wa serikali uzorote.”
Kwa mujibu wa takwimu, kila mwaka takriban kontena 14,000 husafirishwa kutoka bandari za Italia na maeneo jirani kuelekea Israel, hivyo, bandari hizo zina nafasi muhimu katika usafirishaji na biashara za Israel.
Chanzo: Middle East Eye
Maoni yako