Jumatano 24 Septemba 2025 - 07:57
Venezuela: Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kuvunja ukimya kuhusiana na Palestina

Hawza/ Serikali ya Venezuela imeutaja uamuzi wa mataifa kadhaa ikiwemo Uingereza, Australia, Kanada na Ureno wa kulitambua taifa la Palestina kuwa ni hatua ya kihistoria, na ikaitaka jumuiya ya kimataifa isibaki kimya bali ichukue msimamo thabiti katika kulinda haki na amani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya  Shirika la Habari la Hawza, Ivan Gil, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, kupitia ujumbe aliouandika kwenye Telegram alitangaza: “Venezuela inakaribisha utambuzi wa dola ya Palestina na idadi inayoongezeka ya mataifa, na inaunga mkono kikamilifu juhudi za mkutano wa kimataifa kwa ajili ya kutekeleza suluhu ya mataifa mawili.” Imetarajiwa kwamba sambamba na kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, kutafanyika mkutano wa kufufua mjadala wa kuundwa kwa dola mbili — Palestina na Israel.

Caracas, ikisisitiza juu ya “mshikamano usiotetereka” wake na taifa la Palestina, iliitaka jumuiya ya kimataifa “kuvunja ukimya na kusimama kwa uthabiti katika kutetea haki, mamlaka na amani.” Serikali ya Venezuela pia ililaani “mauaji ya kimbari ya kimfumo” yanayoendelea katika Ukanda wa Ghaza, ambako Israel tangia Oktoba 2023 imeendesha operesheni kubwa za kijeshi zilizosababisha maelfu ya watu kuuawa na mamia kutekwa nyara.

Serikali ya Nicolás Maduro ilieleza vitendo vya Israel kuwa ni “msiba wa kibinadamu” unaoweza kulinganishwa tu na uhalifu wa mauaji ya kimbari ya Wanazi, wakati huohuo, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, baada ya wimbi la mataifa kuitambua Palestina, alisisitiza: “Hakutakuwa na dola ya Palestina.”

Kwa upande mwingine, mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na Uingereza — washirika wa jadi wa Israel — waliipa Tel Aviv onyo la kutochukua hatua yoyote ya kisasi dhidi ya uamuzi huu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha