Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, katika salamu na pongezi zilizotumwa na wananchi, magavana, mawaziri, viongozi wa taasisi na maafisa mbalimbali kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Yemen, Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi, kutokana na mnasaba wa kumbukumbu hiyo ya mwaka wa kumi na moja, wote kwa pamoja wametambua mapinduzi haya kuwa ni lango halisi la kujitegemea Yemen dhidi ya ubeberu na ushawishi wa kigeni.
Viongozi hao katika salamu zao wamekazia kwamba mapinduzi haya hayakuwafukuza mamluki pekee, bali pia yameiweka Yemen shujaa katika mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya ukafiri na maadui wa Kiamerika na Kizayuni.
Vyama vya kisiasa vya Yemen, kwa pamoja katika taarifa yao, vimetangaza kuwa mapinduzi haya ni dhihirisho la kweli la azma huru ya wananchi wa Yemen, wamesema kujitolea kwao katika muongo mmoja wa vita, kumeifanya Yemen kuwa na nafasi ya kipekee na ya kuamua mustakabali wa eneo hili leo.
Mapinduzi ya tarehe 21 Septemba nchini Yemen yaliiondoa serikali ya Ali Abdullah Saleh chini ya uongozi wa Ansarullah, na kuiangamiza mizizi ya miaka mingi ya udikteta, ubeberu na kuingilia Marekani pamoja na mataifa ya kigeni.
Kwa sasa, mapinduzi haya yanapoingia muongo wake wa pili wa ustawi, Yemen imekuwa nguvu kuu katika mapambano dhidi ya adui Muisraeli na katika Bahari Nyekundu.
Chanzo: Al-Masirah
Maoni yako