Jumanne 23 Septemba 2025 - 21:57
Maandamano makubwa yakibeba kaulimbiu isemayo “Watoto wa Ghaza” yamefanyika katika mji wa Karachi, Pakistan

Hawza / Maandamano makubwa yaliyobeba kaulimbiu isemayo “Watoto wa Ghaza” yamefanyika mjini Karachi, Pakistan; mamilioni ya watoto, wanafunzi wa shule na wanafunzi wa vyuo walishiriki kwa wingi na kuonyesha mshikamano wao na watoto wa Kipalestina.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, chama cha Jamaat-e-Islami Pakistan kiliandaa maandamano makubwa kwa anuani ya “Watoto wa Ghaza” mjini Karachi, katika hafla hii, mamilioni ya wanafunzi wa shule, wanafunzi wa vyuo na watoto walihudhuria na kutangaza mshikamano wao na taifa la Palestina.

Maandamano haya yalifanyika katika barabara ya Qaidin kwa ajili ya kupinga mashambulizi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina, hususan watoto wasio na ulinzi, washiriki walipaza sauti kwa kusema “Labbaik ya Aqsa” na “Labbaik ya Ghaza” huku wakitangaza uungaji mkono wao kwa Palestina na muqawama dhidi ya hatua za Marekani na Israel.

Vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa viliripoti kwa mapana maandamano haya na kuyataja kuwa maandamano makubwa na ya kipekee zaidi katika historia ya Karachi.

Wanafunzi wa shule na vyuo, huku wakiwa wamevaa mavazi ya aina moja, na kubeba bendera za Palestina na mabango yanayoonesha uungaji wao mkono, waliibadilisha barabara ya Qaidin kuwa uwanja wa mshikamano na umoja.

Mwisho wa hafla, Hafidh Naeem-ur-Rehman, kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan, katika hotuba yake alishukuru kwa uwepo mkubwa wa wananchi hususan vijana, na akasisitiza juu ya ulazima wa kuwaunga mkono watoto wa Palestina na kusimama imara dhidi ya dhulma ya utawala wa Kizayuni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha