Jumapili 14 Septemba 2025 - 00:27
Harakati ya Umma yalaani kukengwa viongozi wa Hamas huko Doha

Hawza/ Harakati ya Umma nchini Lebanon imelaani vikali uvamizi wa Kizayuni dhidi ya kikao cha viongozi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu Hamas kilichofanyika mjini Doha, mji mkuu wa Qatar.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Harakati ya Umma katika tamko lake imelaani vikali uvamizi wa Kizayuni dhidi ya kikao cha viongozi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu Hamas mjini Doha, mji mkuu wa Qatar, na kulitaja tukio hilo kuwa ni “tendo la kigaidi kwa maana kamili ya neno”.

Harakati hii imesisitiza kuwa shambulizi hilo ni uvunjaji wa wazi wa sheria na kanuni zote za kimataifa na linapuuza kwa dhahiri viwango na msingi ya kibinadamu.

Harakati ya Umma imesema kuwa uvamizi huo umetokea katika wakati ambapo Doha ilikuwa mwenyeji wa ujumbe kutoka kwa utawala wa Kivamizi kwa ajili ya mazungumzo, jambo linaloongeza hatari ya kisiasa na kidiplomasia mara dufu.

Harakati hii mwishoni imesema: shambulizi hili la kinyama linathibitisha kuwa utawala wa Kizayuni umedhamiria kuendelea na vita vyake vya maangamizi dhidi ya watu wa Palestina, hili ni jambo hatari sana ambalo halipaswi kuvumiliwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha