Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah ya Lebanon katika tamko lake la kulaani shambulio la leo la utawala wa Kizayuni mjini Doha ilieleza: “Uhalifu huu wa kigaidi na wa woga wa kitoto ni ushahidi unao onesha uovu na udhalili wa utawala wa Kizayuni, ambao kwa kufunua sura mpya ya jinai, umevunja sheria na mikataba yote ya kimataifa, utawala huu hauna heshima yoyote kwa mamlaka ya nchi nyingine, na kwa msaada kamili wa Marekani, bila kizuizi chochote, unaendelea kuvunja sheria.”
Hizbullah ikasisitiza kuwa: “Shambulio hili, lililofanyika wakati wa kikao cha kujadili mpango wa karibuni wa Marekani, linathibitisha wazi kwamba utawala wa Kizayuni si mtafutaji wa mazungumzo wala suluhisho, bali unafuatilia tu kuendeleza miradi yake yenye damu ambayo msingi wake ni mauaji, uharibifu na maangamizi – hata kama hatua hizo zitaligharimu maisha ya mateka wake wote, hatua hii ni kutangaza wazi dhamira ya utawala huu ya kufanya mauaji, umwagaji damu, uhamishaji wa lazima, uharibifu wa kimfumo na mauaji ya kimbari huko Ghaza, Ukingo wa Magharibi na katika nchi nyingine za eneo hili.”
Hizbullah imezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu pamoja na jamii ya kimataifa zichukue hatua za haraka kusitisha mauaji haya ya kila siku na kuulazimisha utawala wa Kizayuni kubeba dhima ya matendo yake, aidha, imesisitiza kwamba badala ya kuishia katika kauli za kukemea na kulaani pekee, nchi hizo zinapaswa kukata uhusiano wao wote na utawala huu ghasibu, na kuilazimisha Marekani kwa njia mbalimbali kusitisha msaada wake usio na kikomo kwa adui huyu, kabla ya miradi ya kikoloni ya utawala huu – ambayo imetangazwa waziwazi – haijawa uhalisia wa kulazimishwa na wa kuangamiza kwa eneo na watu wake.
Mwisho wa tamko hilo ilisisitiza: “Uvamizi huu utaimarisha zaidi azma ya taifa la Palestina ya kushikamana na chaguo la muqawama na kusimama imara katika kutetea ardhi yao, hata kama gharama na kujitolea vitakuwa vikubwa.”
Wakati huohuo, nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu pamoja na mashirika ya kimataifa yamelilaani vikali shambulio hili la utawala wa Kizayuni mjini Doha, na kulieleza kuwa ni uvunjaji mkubwa wa sheria za kimataifa na tishio kubwa kwa mamlaka na usalama wa Qatar.
Maoni yako