Kwa mujibu waShirika la Habari la Hawza, katika matukio mapya ya eneo hili, ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni zimeshambulia moja ya meli za msafara wa “Sumud” iliyokuwa imewabeba wapigania uhuru kutoka nchi 44 duniani, shambulio hili limeibua upinzani na hisia kali katika sehemu mbalimbali, wakati ambapo tangu jana zaidi ya majengo 50 ya makazi yamebomolewa katika Ukanda wa Ghaza, huku watu wote wamesalia wakiwa na mshangao mbele ya unyama huu.
Kuhusiana na jambo hili, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, zaidi ya miaka 15 iliyopita (mwaka 1389 Hijria Shamsia / 2010), akirejelea umuhimu wa msaada wa kimaonyesho kwa Ghaza alisema: “Kitendo cha mfano na chenye mwangaza cha kutuma msafara wa majini kuelekea Ghaza kinapaswa kurudiwa mara nyingi katika sura na njia mbalimbali, Serikali dhalimu ya Kizayuni na waungaji mkono wake, hususan Marekani na Uingereza, wanapaswa kuuona na kuuhisi uwezo usioweza kushindwa wa azma na mwamko wa dhamira ya umma wa dunia.”
Shambulio hili limeibua upya maswali makubwa kuhusiana na haki za binadamu, namna ya kukabiliana na uvamizi na dhulma katika ngazi ya kimataifa, na limezidisha wito wa mshikamano na mwitikio wa wapenda haki duniani kote, wengi sasa wanauliza: Ikiwa maisha ya watu kutoka mataifa mengi yako hatarini, ni vipi tena ulimwengu unaweza kufumbia macho uovu huu wa wazi?
Mwisho wa taarifa
Maoni yako