Jumamosi 30 Agosti 2025 - 09:26
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu: Umoja wa Waislamu na suala la Palestina ni miongoni mwa misingi madhubuti katika itikadi za madhehebu ya Kiislamu

Hawzah/ Hafidh Naeemur-Rahman, Amir wa Jamaat-e-Islami Pakistan, akiwa ameongozana na ujumbe wa ngazi ya juu kutoka chama hicho, alihudhuria katika Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu na kukutana na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Dkt. Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, ambapo walijadili masuala muhimu kuhusu mshikamano wa ulimwengu wa Kiislamu na uungaji mkono kwa Palestina

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kutoka Tehran, Hafidh Naeemur-Rahman, Amir wa Jamaat-e-Islami Pakistan, pamoja na ujumbe wa ngazi ya juu wa chama hicho, walihudhuria kikao hicho na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya, na kujadiliana kuhusu masuala muhimu ya mshikamano wa ulimwengu wa Kiislamu na msaada kwa Palestina.

Katika kikao hicho, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Shahriari, akifafanua hali ya Iran baada ya vita vya siku 12, aligusia kufanyika kwa Kongamano la 39 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu nchini Iran na akasema: “Rais wa Iran atashiriki katika kongamano la mshikamano wa mwaka huu, na tunakualikeni mshiriki katika Kongamano la 39 la Umoja wa Kiislamu nchini Iran.”

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shahriari, akiashiria nafasi ya Jamaat-e-Islami Pakistan, alisisitiza: “Chama hiki ni miongoni mwa vyama mashuhuri zaidi katika Bara Dogo, na fikra za Muasisi wake, Sayyid Abul A‘la Maududi, zinafanana sana na fikra za Imam Khomeini (r.a.).”

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu vilevile aligusia tunu tatu kuu za Uislamu na akabainisha: “Madhehebu ya Kiislamu, kwa kuzingatia misingi mikuu mitatu ya usalama, uadilifu na heshima ya utu katika Uislamu, ndiyo yanayowafanya Waislamu waguswe kwa kina na suala la Palestina.”

Katika sehemu ya maneno yake, alishukuru misimamo ya Jamaat-e-Islami Pakistan kuhusu kuunga mkono Palestina na akasema: “Huu ni wajibu wa kibinadamu, na mshikamano wa ndani wa Pakistan baada ya vita vya siku 12 ilikuwa moja ya mafanikio makubwa ya vita hivyo, hata baadhi ya wale ambao huko Pakistan hawakuwa pamoja nasi, katika vita vya kulazimishwa vya siku 12 walitoa taarifa kwa manufaa yetu, na hili ni jambo kubwa.”

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Shahriari alisisitiza: “Saudi Arabia ilitangaza kwamba haitaruhusu ndege za Marekani kutumia ardhi yao kwa ajili ya kuivamia Iran, na mshikamano huu wa ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya Israel ni thamani, na sisi tunalithamini hili na tunajitahidi kulipanua.”

Hafidh Naeemur-Rahman naye katika kikao hicho alieleza kuwa Iran imefaulu katika mtihani wa kimbinguni wa hivi karibuni katika vita vya siku 12, na akashukuru jitihada za Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu kwa ajili ya kuunda mshikamano miongoni mwa Waislamu.

Akaongeza: “Wale ambao hapo awali hawakujali mshikamano, baada ya vita vya Ghaza waligundua kwamba hakuna njia nyingine isipokuwa mshikamano.”

Amir wa Jamaat-e-Islami Pakistan, ambaye amefanya safari yake kwa mwaliko wa Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu, alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa madhehebu nchini Pakistan na ushirikiano na Iran ili kukabiliana na mipasuko ya kimadhehebu na kuimarisha mshikamano miongoni mwa Waislamu.

Pia alitangaza uungaji mkono kamili wa chama chake kwa sera za Iran kuhusu Palestina na upinzani wake dhidi ya kutambuliwa kwa Israel, na akasema: “Misimamo yetu inajengeka juu ya haki na batili, Jamaat-e-Islami Pakistan si chama cha kawaida; sisi tunafanya kazi kwa ajili ya kusimamisha dini na kukabiliana na mgawanyiko wa madhehebu huko, na tunataka kusaidiwa katika uwanja huu.”

Nae Naeemur-Rahman, akiashiria matatizo ya nchi za Kiislamu kuhusu Palestina, alisema: “Hali ya Palestina ni fursa ya mshikamano wa ulimwengu wa Kiislamu, na ni lazima taasisi na serikali za Kiislamu zishirikiane katika uwanja huu.”

Aidha alisisitiza haja ya kuutambulisha Uislamu na thamani zake kwa vijana wa Magharibi kama nguvu ya kiroho na akataka kuwepo ushirikiano kati ya Iran na Pakistan katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Mwisho wa ujumbe

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha