Ijumaa 29 Agosti 2025 - 17:44
Ayatullah A‘rafi akutana na Waziri Mkuu wa Malaysia / Sera ya Serikali na Watu wa Malaysia ni kuliunga mkono taifa la Palestina lililodhulumiwa hususan Gaza

Hawzah/ Mkurugenzi wa Hawzah nchini Iran pamoja na ujumbe alioambatana nao wakiwa na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Malaysia walikutana na Mheshimiwa Anwar Ibrahim, Waziri Mkuu wa nchi hiyo

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Habari za Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawzah Irn, pamoja na ujumbe alioambatana nao, na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Malaysia, walikutana na Mheshimiwa Anwar Ibrahim, Waziri Mkuu wa Malaysia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo: Katika mkutano huu uliofanyika katika mazingira ya urafiki na maelewano, Mkurugenzi wa Hawzah alitoa pongezi kwa Waziri Mkuu wa Malaysia kwa maadhimisho ya mwaka wa 1500 wa kuzaliwa Mtume wa Uislamu (s.a.w) na pia kwa Siku ya Uhuru wa Malaysia, na akamshukuru kwa misimamo yake mizuri kuhusu ulimwengu wa Kiislamu, hususan misimamo yake ya kuwatetea watu wa Palestina waliodhulumiwa na wananchi wa Ghaza.

Mkurugenzi wa Hawzah, sambamba na kutoa shukrani kutokana na misimamo ya Serikali na Watu wa Malaysia katika kuilinda Iran wakati wa vita vya siku 12, alisema: “Taifa, Serikali na Jeshi la Iran kwa nguvu kamili wamesimama imara dhidi ya uvamizi wowote.”

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawzah za Kielimu alibainisha kwamba utawala wa Kizayuni ni tishio kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu, na akasisitiza kuwa kukabiliana nao kwa pande zote ni jukumu la Waislamu wote.

Ayatullah A‘rafi alieleza kuwa mkakati wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mkakati wa kiumma wa Kiislamu na usio na mipaka ya kimadhehebu, na akasema: “Katika miaka iliyofuata baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, tumekuwa tukisimama pamoja na mataifa yaliyodhulumiwa ya Afghanistan, Bosnia na Palestina, bila ya kuzingatia itikadi zao za kimadhehebu.”

Mkurugenzi wa Hawzah za Kielimu alitaja vita vya siku 12 vya hivi karibuni kuwa, licha ya hasara na madhara yaliyosababishwa, vilikuwa na fursa na matokeo yenye thamani kubwa, na akahesabu mshikamano na umoja wa kipekee baada ya vita hivyo pamoja na mshikamano wa Taifa na Serikali kuwa ni miongoni mwa matokeo muhimu zaidi.

Vilevile aligusia baadhi ya mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan mafanikio ya kielimu na kiutamaduni, na akatoa ripoti kuhusu hali ya sasa ya Hawzah na mafanikio yake. Mwishoni, alitangaza utayari wake wa kupanua mahusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili za Iran na Malaysia.

Katika mkutano huo pia, Mheshimiwa Anwar Ibrahim, Waziri Mkuu wa Malaysia, sambamba na kukaribisha maendeleo ya uhusiano wa nchi mbili katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kitamaduni, kielimu na kadhalika, alisisitiza kuwa sera ya Serikali na Watu wa Malaysia ni kuliunga mkono taifa la Palestina lililodhulumiwa, hususan watu wa Ghaza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha