Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, mkutano huu wa pili wa Kimataifa wa Viongozi wa dini Duniani leo (Alhamisi) umefunguliwa rasmi mjini Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, huku ukihudhuriwa na Ayatollah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, na ujumbe wa wanazuoni pamoja na shakhsia wa kielimu wa Hawza, pamoja na zaidi ya shakhsia elfu moja mashuhuri za kidini kutoka nchi 54 duniani, chini ya kauli mbiu isemayo: “Nafasi ya viongozi wa kidini katika kutatua mizozo.”
Ayatollah Arafi ambaye ameshiriki katika mkutano huu kwa mwaliko rasmi wa "Anwar Ibrahim", Waziri Mkuu wa Malaysia, na Katibu Mkuu wa "Rabita al-‘Alam al-Islami", leo atatoa hotuba yake.
Ratiba ya safari hii, ambayo itaendelea kwa mujibu wa mpangilio ulioainishwa kabla, ni pamoja na kukutana na kufanya mazungumzo na shakhsia za kimataifa, viongozi wakuu wa Malaysia, kutembelea vituo vya kielimu, pamoja na kukutana na Wairani wanaoishi nchini humo na wanafikra wa elimu za kibinadamu na Kiislamu.
Maoni yako