Jumatano 27 Agosti 2025 - 20:41
Ayatollah A‘rafi asafiri kuelekea Malaysia

Hawza/ Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran amesafiri kuelekea Malaysia kutokana na mwaliko wa Waziri Mkuu wa Malaysia akiwa ameandamana na ujumbe maalum

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, pamoja na ujumbe aliokuwa ameandamana nao, wamesafiri kuelekea nchini Malaysia

Safari hii imefanyika kutokana na mwaliko wa pamoja wa Anwar Ibrahim, Waziri Mkuu wa Malaysia, Waziri wa Dini wa nchi hiyo, na Katibu Mkuu wa "Rabitat al-‘Alam al-Islami", kwa ajili ya kushiriki katika “Mkutano wa pili wa kimataifa wa viongozi wa kidini” ukiwa na anuani isemayo: “Nafasi ya viongozi wa dini katika kutatua migogoro.”

Kukutana na shakhsia za kimataifa zilizopo katika mkutano huo na shakhsia za kisiasa na kidini nchini Malaysia, kutembelea vituo vya kielimu na vyuo vikuu, kukutana na Wairani walioko nchini humo na wasomi wa elimu za kibinadamu na Kiislamu, ni miongoni mwa ratiba zilizopangwa kwa ajili ya safari hii.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha