Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, sheikh Abdulatifu Swaleh kwenye ujumbe wake ambao aliutoa katika matembezi hayo alianza na aya ya Mwenyezi Mungu isemayo:
{وَمَا أَرۡسَلنـٰك إِلَّا رَحمة للعَـٰلَمِینَ}
Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.
[Surah Al-Anbiyāʾ: 107]
Katika kuielezea aya hiyo alisema kwamba: Mtume Muhammad (saw) ni Rehma, rehma maana yake ni huruma, upole, na amanai. Katika muendelezo wa mazungumzo yake akasema: Na sisi kwa pamoja tumetoka ili kudhihirisha huruma yetu pamoja na watu wote walio nyongeshwa katika ulimwengu huu, kama vile ambavyo Mtume alisifika kwa amani basi nasi tumefanya matembezi haya ya amani kwa ajili ya kukumbuka kifo chake.
Picha za matembezi hayo ni kama ifuatavyo:
Maoni yako