Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Jeshi la Yemen limetangaza kufanya operesheni tatu maalumu za kijeshi kwa kulenga Uwanja wa Ndege wa “Ben Gurion” katika eneo lililovamiwa la Yafa na malengo mawili ya adui Mwisraeli katika maeneo ya Yafa na Asqalan ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Jeshi la Yemen katika taarifa iliyotolewa leo limeeleza kwamba jeshi la makombora limeendesha operesheni ya kijeshi yenye ubora wa juu kwa kulenga Uwanja wa Ndege wa “Ben Gurion” katika eneo la uvamizi wa Yafa kwa kutumia kombora la masafa ya juu la “Falastin-2”, ambalo limepita mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel.
Jeshi la Yemen limethibitisha kwamba operesheni hiyo imefikia shabaha yake kwa mafanikio, ikasababisha mtafaruku mkubwa miongoni mwa adui Mwisraeli, ikawalazimisha mamilioni ya Wazayuni wavamizi kukimbilia kwenye mahandaki, na kusababisha kusimamishwa kwa shughuli za uwanja wa ndege.
Taarifa hiyo imeongeza kwamba jeshi la anga limefanya operesheni mbili za kijeshi kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drones) na kulenga malengo mawili ya adui Mwisraeli – moja la kijeshi na jingine la kimaisha – katika maeneo ya Yafa na Asqalan ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, imeelezwa kuwa operesheni zote mbili zimefikia shabaha zake kwa mafanikio.
Taarifa hiyo pia imesisitiza kwamba Jeshi la Yemen, pamoja na taifa lote la Yemen, linatoa shukrani kwa mashujaa na wapiganaji watakatifu wenye kusimama imara huko Gaza, ambao wanadhihirisha mfano bora zaidi wa kusimama dhidi ya maadui wa mataifa, na wanaojitolea nafsi zao na kila walicho nacho katika kuilinda heshima na hadhi ya taifa, na katika kukataa miradi ya uvamizi na mipango ya upanuzi.
Maoni yako