Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Abdullah, aliyasema haya alipokuwa akipokea ujumbe wa vyombo vya habari katika Dar al-Ifta’ al-Ja‘fari mjini Sur, wakati ambapo watu na taasisi za Lebanon walishiriki katika Siku ya Mshikamano na Ghaza iliyoandaliwa na Umoja wa Redio na Televisheni za Kiislamu kwa ushiriki mpana wa vyombo vya habari kutoka ulimwengu wote wa Kiislamu.
Sheikh Abdullah alisisitiza kwamba suala la Palestina si janga jipya, bali lina mizizi yake tangu mwaka 1948, wakati wa mwanzo wa Nakba ya uhamishaji na uvamizi, hata hivyo, alibainisha kuwa yale ambayo Ghaza inashuhudia leo ni kilele cha ukosefu wa haki na kushindwa kwa mfumo wa kimataifa.
Akiashiria kushindwa kwa mashirika ya haki za binadamu katika kuzuia uhalifu wa kimbari ulioandaliwa, Sheikh Abdullah alielezea kushindwa huko kama kufilisika kwa maadili.
Mufti wa Sur na Jabal Amel alieleza kwamba; ukimya wa kimataifa hususan kutoka Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa, umekuwa na mchango mkubwa katika kuigeuza Ghaza kuwa uwanja wa mauaji ya taratibu kupitia njaa, kiu na kusambaratika kwa huduma za afya.
Akasema: “Kinachotokea si vita pekee, bali ni vikwazo, njaa na mauaji ya watoto, wanawake na wazee. Hata maeneo yaliyotangazwa kuwa salama yamegeuzwa kuwa maeneo ya mauaji ya kimbari, ukimya huu wa kimataifa si kutokuwa na upendeleo, bali ni ushirikiano wa wazi katika uhalifu huu.”
Sheikh Abdullah alisisitiza kuwa; uhalali wa kimya kimya unaopewa uvamizi wa Israel na mataifa makubwa ni uhalifu mara mbili, kwani unahalalisha mauaji chini ya kivuli cha uongo cha uhalali, alitoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na zenye ufanisi za kimataifa.
Aidha aliziomba, taasisi za kidini na mashirika ya habari kupaza sauti dhidi ya utekaji wa Israel na wale wanaounga mkono uhalifu huo.
Alisisitiza kuwa kinachotokea kitaimarisha zaidi azma ya watu wa nchi hiyo kushikamana na haki na kuwashtaki watekaji kwa kila uhalifu uliofanywa tangu mwaka 1948 hadi leo.
Sheikh Abdullah aliongeza kuwa; Lebanon ambayo bado inateseka kutokana na uvamizi na vitisho vya kila siku vya watekaji wa Kizayuni, inasimama kwa hisia, kisiasa na kwa vyombo vya habari pamoja na watu wa Palestina.
Mwisho, alibainisha kuwa mimbari huru za Lebanon zitabakia kuwa sauti ya kweli mbele ya uvamizi na utelekezwaji kwa kimataifa.
Maoni yako