Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Shafqat Hussein Shirazi, Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, kufuatia matamshi ya vitisho na matusi ya Rais wa Marekani dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mtukufu Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (Mola amuhifadhi), kupitia barua yake ya wazi aliyoielekeza kwa maulamaa, maimamu wa Ijumaa na jamaa, pamoja na wahubiri wa dini, huku akilaani vikali kitendo hicho, alikitaja kuwa ni shambulizi la moja kwa moja dhidi ya nafasi tukufu ya Marjaa na Wilaya.
Katika barua hiyo, alieleza kuwa mtazamo huo wa mfumo wa kibeberu ni wa kishetani, wa hadaa na wa uovu, na akaeleza bayana: Vitisho hivi havielekezwi kwa mtu mmoja tu, bali ni uvamizi dhidi ya taasisi ambayo leo hii ndiyo mhimili wa uongozi wa kidini na kifikra wa Umma wa Kiislamu, mwelekezaji wa mipaka ya haki na batili, na ni alama ya basira, ujasiri na uanaharakati wa kutafuta haki mbele ya dhulma na ubeberu wa kimataifa.
Mwanazuoni huyu wa Kipakistani, huku akisisitiza kuwa uongozi wa Mtukufu Ayatollah Khamenei ni mwendelezo wa kihistoria wa sunna ya Ghadir na Ashura ya Ahlul-Bayt "as", aliongeza kwa kuswma: Nafasi hii takatifu kwa sasa ni tumaini la wanyonge na waliodhulumiwa huko Palestina, Yemen, Lebanon na maeneo mengine duniani, na wakati huo huo ni chombo cha kuwaamsha watu kutokana na mfumo wa kibeberu wa kimataifa.
Maoni yako