Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, utafiti wa maoni unaonyesha kuwa kati ya kila Wamarekani wanne, watatu wao wana wasiwasi kuhusu radi-amali ya Iran kutokana na mashambulizi ya mabomu ya Marekani dhidi ya mitambo ya nyuklia ya Iran.
Kwa mujibu wa utafiti wa maoni uliofanywa na mitandao ya habari ya "PBS News", "NPR" na "Marist", asilimia 75 ya watu wazima wa Marekani walionesha wasiwasi wao au wasiwasi mkubwa juu ya uwezekano wa Iran kulipiza kisasi kwa kuihujumu Marekani kufuatia mashambulizi hayo dhidi ya vituo vitatu vya nyuklia vyake.
Nusu ya Wamarekani walioshiriki katika utafiti huo walieleza upinzani wao kwa mashambulizi ya mabomu ya Marekani dhidi ya Iran, huku nusu nyingine wakiunga mkono mashambulizi hayo.
Alfajiri ya tarehe 22 Juni, Jeshi la Anga la Marekani lilianzisha shambulizi la anga dhidi ya mitambo ya nyuklia ya chini ya ardhi na iliyojengeka kwa uimara ya Iran kwa kutumia mabomu sita ya kupenya miamba, ambapo shambulizi hilo lilifanyika sambamba na mashambulizi ya mabomu ya Israel dhidi ya Iran.
Maoni yako