Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, wanafunzi wa Azerbaijan waliopo Qom, wametoa tamko lao baada ya mashambulizi ya serikali ya ghasbu ya Kizayuni na Marekani kwenye ardhi takatifu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
"Na kwa hakika tumeandika katika Zabur baada ya Torati kwamba ardhi itarithiwa na waja wangu wema."
(Qur’an, Sura Al-Anbiya: 105)
Sisi, wanazuoni wa Jamhuri ya Azerbaijan tunaosoma katika hawza ya Qom, tunakanusha wazi mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na serikali haramu ya Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na vitisho na vitendo vya uchochezi vya maadui wa Uislam dhidi ya Mkuu wa Waislamu, Ayatullah Al-Udhama Imam Khamenei!
Vitendo hivi sio tu ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa, bali pia ni matusi ya moja kwa moja kwa watu watakatifu katika ulimwengu wa kiislamu.
Tunatangaza kwamba sera za udhalimu za serikali ya haramu na njama zake za kuvuruga utulivu wa ukanda huu hazitafanikiwa kamwe.
Tunaamini kwamba umoja wa Kiislamu na mshikamano wa watu wa Kiislamu utakabiliana na kila fitina na uharibifu.
Vitisho dhidi ya Imam Khamenei ni dalili ya udhaifu wa maadui wa Uislam katika uwanja wa vita. Yeye, kama kiongkzi wa Waislamu, ni kielelezo cha roho ya kupigania umma wa Kiislamu, na kila shambulio dhidi yake ni shambulio kwa waislamu wote.
Sisi, wanazuoni wa Jamhuri ya Azerbaijan, tunawataka waislamu wote wawe pamoja, mshikamano, na kuungana kwa nia. Kupambana na uonevu, kuwasilisha sauti za wanyonge ulimwenguni, na kusimama dhidi ya vitisho vinavyoukabili Uislamu ni wajibu wetu wa kidini na kibinadanu.
Tunasisitiza kusimama pamoja na upande wa haki katika vita hivi vya wazi kati ya haki na batili, na kwa matumaini makubwa kwa msaada na neema za Mwenyezi Mungu, tunaamini kwa ushindi wa karibu na wa hakika!
"Na ilikuwa ni haki yetu kuwanusuru Waumini."
(Qur’an, Sura Ar-Rum: 47)
Wanazuoni wa Jamhuri ya Azerbaijan
Hawza ya Qom
Maoni yako