Jumamosi 14 Juni 2025 - 21:17
Shambulio dhidi ya Iran ni shambulio dhidi ya ulimwengu wa kiislamu

Hawza/ Hujjatul-Islam Maqsuud Ali Domki, katika khutba ya Swala ya Ijumaa, huku akilaani mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, alitaja hatua hizo kuwa ni uvamizi dhidi ya uislamu ulimwenguni kote, na akasisitiza juu ya ulazima wa umoja wa Umma wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Maqsuud Ali Domki, Katibu Mkuu wa Masuala ya Uchapishaji na Utoaji Habari wa Bunge la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, na Mwenyekiti wa Baraza la Uandishi wa Mitaala ya Elimu ya taasisi hiyo, katika khutba ya Swala ya Ijumaa katika mji wa Multan, Pakistan, huku akisisitiza mshikamano wa Umma wa Kiislamu mbele ya utawala wa Kizayuni, alieleza kuwa: Shambulio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran si uvamizi tu dhidi ya ardhi ya nchi moja, bali linahesabiwa kuwa ni uvunjaji wa heshima tukufu ya uislamu duniani kote.

Utawala wa Kizayuni, kwa kufanya mashambulizi dhidi ya Palestina, Ghaza, na sasa Iran, unajitahidi kuharibu heshima na hisia za utu za Umma wa Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha