Jumamosi 31 Mei 2025 - 09:10
Hawza haijajitenga mbali na siasa

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza amesema kuwa, maandalizi ya wanafunzi wa elimu ya dini (talaba) yanapaswa kufanyika kwa haraka, na akasisitiza kuwa: "Ili kufanikisha lengo hili, hatupaswi kupunguza kiwango cha ubora wa elimu, bali mbinu za kufundisha ndizo zinapaswa kubadilishwa."

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Mohsen Araki, katika siku ya pili ya kikao cha viongozi wa Hawza za mikoa na manaibu pamoja na wakurugenzi wa ofisi kuu ya uongozi wa Hawza, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaamiatul Al-Mustafa mjini Qom, alisema: "Kongamano la miaka mia moja ya Hawza za Kiislamu linaweza kuitwa kuwa ni tukio lenye kuleta mageuzi makubwa."

Akaongeza kuwa: "Sababu ya msisitizo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Ayatollah Khamenei) juu ya mageuzi katika Hawza ni kwamba; Hawza za Kishia hazijawahi kuwa mbali na jamii, bali daima zimekuwa zikijibu mahitaji ya jamii."

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza, huku akibainisha kwamba maulamaa wa Kishia ni warithi wa Mitume na wanabeba majukumu mazito, alisema: "Jukumu letu la kwanza katika uhusiano huu ni kuchunguza matukio ya dunia na jamii yetu."

Akaongeza kuwa: "Matukio haya mara nyingi yanatokana na Shetani, na vita yetu ni vita dhidi ya maadui, si vita dhidi ya watu. Vita hii ni juu ya mamlaka ya Mwenyezi Mungu dhidi ya mamlaka ya Shetani."

Ayatollah Araki, kwa kusisitiza kwamba sisi ni wanajeshi wa mstari wa mbele wa vita hii, alisema: "Katika vita hii, tunajitahidi kuhakikisha kwamba amri ya Shetani haithaminiwi, bali ni amri ya Mwenyezi Mungu ndiyo inayotawala. Na wasambazaji wa amri hii ya Mwenyezi Mungu ni Hawza."

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlisi Khobregan Rahbari) aliendelea kusema: "Kwa hivyo, kama vile dini haijitengi na siasa, vivyo hivyo Hawza haziko mbali na siasa."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha