Jumamosi 17 Mei 2025 - 20:34
Sheikh Ibrahim Zakzaky aomba kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa nchini Nigeria

Hawza/ Sheikh Sayyid Ibrahim Zakzaky amekutana na baadhi ya watu waliokuwa wamefungwa kwa muda wa miaka sita lakini hatimaye wameachiwa huru baada ya kufutiwa mashtaka.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Sayyid Ibrahim Zakzaky amekutana na waliokuwa wafungwa ambao walifungwa kwa miaka sita kwa kosa la kushiriki maandamano ya kudai kuachiliwa kwake. Watu hao walioachiwa huru walimtembelea mara moja kiongozi wa Waislamu wa Kishia nchini Nigeria baada ya kutoka gerezani.

Katika mkutano huu, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria alisema: “Watu 24 kati ya 60 waliokuwa wakishtakiwa katika mahakama ya Abuja wameachiliwa na kufutiwawa mashtaka, ilhali matarajio yetu yalikuwa kwamba ndugu zetu wote waachiliwe huru, kwani kwa mujibu wa taratibu za kiutawala, watuhumiwa hawa walipaswa kuachiwa huru na kufutiwa mashtaka miaka mitatu iliyopita, kwa kuwa hakuna ushahidi wowote dhidi yao.”

Sheikh Zakzaky pia alizungumzia suala la maandamano ya kupinga dhulma na akaeleza kuwa: “Hakuna sheria yoyote inayowazuia wananchi kufanya mikusanyiko ya aina hii au inayowataka kupata kibali kutoka kwa polisi, kwa mujibu wa kauli hii, ndugu zetu hawa hawana kosa lolote na wanapaswa kuachiliwa huru.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha