Ijumaa 16 Mei 2025 - 11:04
Mwanafikra wa Kihindi: Hawza ya Qom ndio Mshika Bendera ya Ijtihadi Dhidi ya fikra mgando

Hawza/ Aqil Reza Turabi, mwanafikra wa Kihindi, katika tamko lake ameielezea Hawza ya Elimu ya Qom kuwa ni mfano wa mapinduzi hai, yenye mwanga, kiroho na kiakili.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Aqil Reza Turabi, mwanafikra wa Kihindi na mkuu wa shule ya Bintul Huda katika jimbo la Haryana, India, katika tamko lake ameitaja Hawza ya Elimu ya Qom kuwa ni alama ya mapinduzi hai, yaliyojaa nuru, uhai wa kiroho na fikra.

Katika ujumbe wake imeelezwa hivi: Karne hufuatana moja baada ya nyingine, na msafara wa zama huendelea kusonga bila mapumziko. Hata hivyo, katika mchakato huu usiokoma, taasisi na fikra fulani huibuka ambazo huacha athari zao zisizofutika katika kurasa za historia, athari ambazo hata vumbi la muda halina uwezo wa kuzifuta. “Hawza ya Qom” ni miongoni mwa taasisi hizo zenye mizizi na zenye athari, ambayo historia imeitaja kwa heshima na kuitukuza, na daima imeinamia mbele ya ukubwa wake wa kielimu na kiroho.

Hawza ya Qom si mkusanyiko tu wa kuta na milango, bali ni mwendelezo wa mila tukufu ya nuru ambayo kuanzia Maktaba ya Baghdad katika karne za kati, hadi mitaa ya Najaf na Mashhad, na hadi kwenye viwanja vya Qom, imeacha athari zake. Hii ndiyo hawza iliyonyanyua bendera ya fikra mpya mbele ya udumavu wa fikra, ikapambana na udumavu wa akili, na ikasimama kama "tamko la haqq" mbele ya dhulma ya watawala.

Qom ni ardhi ambayo imelea watu wa elimu na vitendo; wanaume ambao hawakuhubiri tu juu ya mimbari, bali waliwaongoza watu katika mihrabu, wakafundisha katika madrasa, wakashahidi katika uwanja wa mapambano, na wakapanda mbegu za mwamko ndani ya mataifa. Kuanzia jihadi ya Imam Khomeini (ra) hadi kalamu ya Shahidi Murtadha Mutahhari, kutoka kwa kimya cha kiarif cha Ayatollah Bahjat (ra) hadi msisimko wa kielimu wa Ayatollah Subhani, kila mmoja wao ameongeza sura mpya katika ukubwa wa Hawza ya Qom.

Mimi, kwa unyenyekevu kamili, nakiri kwamba Hawza ya Elimu ya Qom, si tu ndani ya Iran, bali pia katika bara la Hindi, Afrika, Ulaya na Amerika, imeacha athari za kina kielimu. Sisi ni wanafunzi kutoka bara dogo la India ambao kwenye ndoto zetu tunaona, Qom hung’aa kama kibla, na mwanga wa fikra zetu huakisiwa kutoka kwenye mandhari yenye nuru ya Qom.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha