Ijumaa 16 Mei 2025 - 11:14
Tamasha la kimataifa la Qur'ani kufanyika nchini Tanzania

Hawza/ Tamasha la kimataifa la Qur'ani limepangwa kufanyika nchini Tanzania huku likishirikisha Taasisi nne mashuhuri nchini humo.

 Shirika la Habari la Hawza - Tamasha kubwa la kimataifa limepangwa kufanyika nchini Tanzania. Tamasha hilo ambalo litakuwa chini ya usimamizi wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Jumuiya ya Amani na Maridhiano (JAMT), Kituo cha utamaduni cha Irani pamoja na Chuo cha Almustafa international.

Tamasha hilo ukiachilia mbali kushirikisha wasomi mahiri kutoka nchini humo, pia watakuwepo magwiji wa kusoma Qur'ani kutokea nchi nyengine kama vile Irani. Tamasha hilo la aina yake limepangwa kufanyika siku ya Alhamisi, taehe 22 mei 2025 nchini Tanzania.
Nyote mnakaribishwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha