Jumatatu 12 Mei 2025 - 13:40
Watalii kutoka Poland wahudhuria Haram ya Bibi Mtukufu mwenye Karama

Hawza/ Watalii 40 kutoka nchi ya Poland, wamehudhuria katika haram takatifu ya Bibi Fatima Maasuma Salamullahi ‘Alayha, kutokana na kuhudhuria kwao waliweza kuifahamu shakhsia na hadhi ya Bibi huyo pamoja na utamaduni na historia halisi ya Kiirani inayohusiana na haram hiyo tukufu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, kwa kushirikiana na idara ya kimataifa ya haram tukufu ya Bibi wa Karama, semina maalumu kwa ajili ya kuifahamu haram ilifanyika kwa ajili ya watu 40 miongoni mwa watalii wa nchi ya Poland ndani ya haram ya Bibi wa Karama.

Kundi hili la Kipolandi, pamoja na kutembelea usanifu wa majengo ya eneo takatifu la Bibi Fatima Maasuma Salamullahi ‘Alayha, lilifahamiana pia na shakhsia na hadhi ya Bibi huyo kama mwanamke wa kipekee kutoka katika kizazi cha Ahlul Bayt ‘Alayhimus-Salaam ambaye kwa kuwepo kwake katika mji mtukufu wa Qom, amekuwa mhimili wa maendeleo ya elimu katika mji huu.

Lengo la kuandaa safari za kuifahamu haram kwa ajili ya watalii wa kigeni ni kuwafahamisha kuhusu sehemu mbalimbali za haram ya Bibi wa Karama, pamoja na kuwapa uelewa kuhusu utamaduni na usanifu wa asili wa Kiislamu Irani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha