Ijumaa 9 Mei 2025 - 00:03
Je! Endapo Hawza na maulamaa wasingekuwepo, katika Uislamu kingelibakia chochote?

Katika nukuu yake, Katibu wa Baraza Kuu la Hawza alisema: Katika kipindi chote cha harakati za Ma’imamu watoharifu (ʿalayhim al-salām), fursa kubwa ya kueneza maarifa ya Kiislamu haikupatikana. Hivyo basi, lau hizi hawza tukufu, maulamaa na wanazuoni katika pembe zote za dunia wasingekuwepo, je! Chochote kingelibakia katika Uislamu?

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Shab Zendehdor leo katika kikao chake na kundi la maulamaa kutoka India waliofika Iran kwa ajili ya kushiriki katika kongamano la kimataifa la kuadhimisha miaka mia moja tangu kurejeshwa kwa Hawza ya Qom, alisema: Kuna riwaya isemayo:

"" اسلام محمدی الحدوث و حسینی البقاست",

" yaani: “Uislamu ulianzishwa na Muhammad na umeendelea kuwepo kwa sababu ya Husein,”

kwani mambo yalikuwa yamefikia mahali ambapo Bwana wa Mashahidi (ʿalayhi al-salām) alisema:

«إِنَّا لِلَّهِ وَ إِنَّا إِلَیْهِ راجِعُونَ‏ وَ عَلَی الْإِسْلَامِ السَّلَامُ إِذْ قَدْ بُلِیَتِ‏ الْأُمَّةُ بِرَاعٍ‏ مِثْلِ یَزِیدَ» 

wakati ambapo Umma wa Muhammad (saw) umepatwa na mtihani wa kuwa chini ya uongozi wa mtu kama Yazid, basi Uislamu uwe umefikia mwisho wake. Na lau isingekuwa kwa ajili ya harakati ya Ashura, basi Uislamu ungepotea katika giza.

Mjumbe wa mafaqihi katika Baraza la Kulinda Katiba alieleza: Katika kipindi chote cha mapambano ya Ma’imamu watoharifu (as), haikupatikana fursa kubwa ya kueneza maarifa ya Kiislamu. Hivyo basi, kwa hakika, lau hizi hawza tukufu, maulamaa na wanavyuoni katika pembe zote za dunia wasingekuwepo, je, chochote kingelibakia katika Uislamu?

Ayatollah Shab Zendedar alisisitiza: Inadhihirika wazi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakupanga kuilinda dini ya Uislamu kwa miujiza, bali lau hawza hizi zisingekuwepo, basi dini ingepotea. Ni hawza na maulamaa ndio walioinua taa na bendera ya Uislamu, na katika sehemu mbalimbali za dunia wamewezesha kubakia kwa madhehebu ya Kishia na dini ya Kiislamu.

Akaongeza: Leo hii, bila shaka, jukumu la maulamaa na askari wa Imamu wa Zamān (a.f) ni kujizatiti kwa zana na mbinu zilezile zinazotumiwa na mahasimu wetu dhidi yetu. Ni lazima tuyafikishie mataifa yote maarifa yetu ya kidini na tutumie zana zote na mbinu zote kwa ajili ya hilo.

Ayatollah Shab Zendedar, akihitimisha, kwa kubainisha kwamba harakati za maulamaa nchini India zina thamani kubwa mno, alisisitiza: Mkusanyiko huu wa juhudi unaandaa njia ya Mapinduzi ya Kimataifa ya Hujjat al-Islam al-Mahdi (ʿajjalallāhu farajahu al-sharīf). Uandaliwaji huu wa ulimwengu kwa ajili ya kuja kwa Bāqiyyatullāh (ʿajjalallāhu farajahu al-sharīf) ni matunda ya juhudi za jihadi za maulamaa na hawza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha