Jumanne 22 Aprili 2025 - 17:33
Ujumbe wa Raisi wa Shura ya Maulamaa wa Kishia Pakistan kutokana na Mnasaba wa kufariki Papa Francis

Kwa mujibu wa shirika la habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Raidi wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, ameeleza masikitiko yake na huzuni kufuatia kifo cha Papa Francis, kiongozi wa jamii ya Wakatoliki duniani.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Raisi wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, kufuatia kifo cha Papa Francis, kiongozi wa jamii ya Wakatoliki duniani, ameonesha huzuni na masikitiko.

Kutokana na tukio hili amesema kwamba: “Sisi tupo pamoja na jamii ya Kikristo katika hili, na tunawapa pole kutokana na msiba huu mkubwa.”

Papa Francis daima katika hotuba zake alikuwa akipinga misimamo mikali, na alichukua nafasi adhimu katika kueneza amani, uvumilivu na kuishi kwa maelewano baina ya dini mbalimbali.

Inafaa kutajwa kwamba Papa Francis (Jorge Mario Bergoglio), kiongozi wa kiroho wa kanisa katoliki wa duniani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88. Vatikani kupitia tamko rasmi, ilitangaza habari ya kifo chake. Papa Francis alikuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa Katoliki kutoka Amerika ya Kusini, na alifariki dunia baada ya kuugua mda mrefu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha