Jumanne 22 Aprili 2025 - 17:34
Ujumbe wa Rambirambi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Vatikani kutokana na Mnasaba wa Kifo cha Papa Francis

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Vatikani ametoa ujumbe wa rambirambi huku akielezea masikitiko yake juu ya kifo cha Papa Francis, kiongozi wa Katoliki duniani.

Kwa mujibu wa idara ya habari ya kimataifa ya  Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Hussein Mokhtari, Balozi wa Iran Vatikani, kwenye ujumbe wake, ametoa salamu za rambirambi kwa Kanisa Katoliki, Serikali ya Vatikani, na Wakristo wote duniani kutokana na msiba wa kifo cha Papa Francis.

Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Kwa masikitiko na huzuni kubwa, nawasilisha rambirambi zangu kwa viongozi wa Vatikani, jamii ya Wakristo, na wafuasi wa marehemu huyo mashuhuri, kutokana na kifo cha Mheshimiwa Papa Francis, kiongozi wa kidini na kiroho wa kanisa katoliki duniani.

Papa Francis daima alikuwa mtu wa kuhamasisha, mpenda amani, na mtetezi wa maadili ya kibinadamu na maadili mema, ambaye jitihada zake katika kukuza mazungumzo baina ya dini, mshikamano wa kimataifa, na uungaji mkono kwa wanyonge, zitabaki katika kumbukumbu ya walimwengu.

Mimi, kwa niaba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, natoa pole za dhati kwa viongozi wa Vatikani na wafuasi wote wa Kanisa Katoliki, huku nikiomba marehemu huyo mwenye heri apumzike kwa amani, pamoja na subira na faraja ziwafikie wafiwa na wapenzi wake.

Muhammad Hussein Mokhtari

Balozi mwenye mamlaka kamili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Makao Matakatifu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha